Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, February 8, 2017

YUSUFU MANJI, ATAJWA KWENYE SAKATA LA DAWA ZA KULEVYA

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda amewataja watuhumiwa 65 wa Dawa  za Kulevya, katika majina hayo ametajwa Freeman Mbowe, Mchungaji
Gwajima, Yusuf Manji, Idd Azzan.

Akizungumza na waandishi wa habari Ofisi kwake mapema leo jijini Dar, Makonda  ameingia katika awamu ya pili ya kutaja majina hayo na kuyaweka hadharani,huku akieleza kuwa watuhumiwa hao watatakiwa kufika kituo cha polisi kati  siku ya Ijumaa,saa tano asubuhi kwa mahojiano zaidi.

Katika hatua nyingine RC Makonda amekiri kukamatwa kwa Mmiliki wa kituo cha
Radio ya EFM,ajulikanae kwa jina la Francis Ciza,almaarufu kwa jina la Dj
Majay.
"tulipokuwa tukifanya opereseheni ya kuwakamata wahusika wote wa Dawa za kulevya juzi usiku nae akakamatwa kwa mahojiano zaidi;"alisema Makonda.

Makonda amejibu habari za kukamatwa kwa Dj Majay mara baada ya kuulizwa swali na mmoja wa waandishi wa habari,kufuatia tetesi nyingi zilizokuwa zikisambazwa kwenye  mitandao mbalimbali ya kijamii.
Soma zaidi majina ya watuhumiwa wa sakala hilo la Dawa za kulevya.