Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, February 8, 2017

TAMASHA LA SAUTI ZA BUSARA KUANZA KURINDIMA KESHO



TAMASHA la Sauti za Busara 2017, Ijumaa litaendesha mafunzo ya sanaa inayohusu fursa za mitandaoni,  changamoto na vitisho vinavuyoigusa tasnia ya muziki.
Akizungumza na gazeti hili Mkurugenzi wa tamasha la Sauti za Busara Bw.Yusuf Mahmoud alisema kwa kutambua uwezo wa kidigitali ni muhimu kwenye taaluma, wahudhuriaji wakajifunza  nguvu ya mitandao ya kijamii ilivyo na nguvu ya kuunganisha mashabiki na wawekezaji, na kuongeza masoko kwa kutumia mitandao ya kijamii.
“Wanamuziki  hujikuta mstari wa mbele kwenye harakati kwa kutumia sauti zao kwa niaba ya wasiosikika wakati mwingine wasanii hujikuta hatarini baada ya ujumbe wa muziki wao kuwatuhumu wasikilizaji na wenye mamlaka,” alisema Mahmoud.
Pia Mahmoud alisema msanii anaweza kutumia uhuru wa kuongea  na kufungiwa kitaaluma ni mada ambayo itaeleza mtazamo huru wa ubunifu Afrika.
Jumapili wasanii wanakaribishwa  kwa maswali na majibu ya kina na ni sehemu ya kipekee  kwa wasanii kutoka bara la Afrika na sehemu mbalimbali kukutana na kubadilishana mawazo.
Kuingia ni kwa mwaliko tu hivyo wasanii na mameneja  wa ndani  wanahamasishwa kuwasiliana na  waandaaji wa  tamasha la Sauti za Sauti za Busara kama watapenda kushiriki.
Tamasha la Sauti za Busara 2017 linatarajiwa kuanza leo hadi Februari 12 Mji Mkongwe, Zanzibar.

No comments:

Post a Comment