Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, February 11, 2017

KLOPP NA NDOTO ZA KUTWAA UBINGWA EPL 
Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amewapa matumaini mapya mashabiki wa timu hiyo katika michezo 14 ambayo imesalia kabla ya kumaliza msimu watashinda michezo na kuiweka klabu hiyo katika nafasi nzuri kushinda ubingwa au kupata nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Liverpool kwa sasa ipo nafasi ya tano ikiwa na alama 46, nyuma ya Chelsea yenye 13, lakini Klopp amesema katika soka kila jambo linawezekana na imani yake ni kushinda michezo yote 14 ambayo ipo mbele yao.
Katika ndoto zangu tunaweza kushinda michezo 14, najua inaweza kupokelewa tofauti lakini siwezi kubadili na hilo ndilo ninalolifanyia kazi na baada ya michezo 14 utakuwa muda wa kuangalia nini tumejifunza kutoka kwa wengine halafu tutafanya maamuzi ambayo yanaweza kutusaidia kwa msimu ujao,” alisema Klopp.

 Ndoto ya Klopp itaanza leo usiku wakati Liverpool itakapokuwa mwenyeji wa Tottenham kwenye uwanja wa Anfield, Tottenham wao wana alama 50 na wakiwa nafasi ya pili ya msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza.