Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, February 11, 2017

RATIBA YA MECHI ZA WIKIENDI HII VPL, LIGI DARAJA I, LIGI DARAJA LA II

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), inatarajiwa kuendelea leo kwa mechi nne kabla ya Jumapili Februari 12, mwaka huu kuendelea kwa michezo mitatu katika viwanja mbalimbali hapa nchini.
Stand United inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa CCM Kambarage, Shinyanga wakati Simba itaikaribisha Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam huku Ndanda ikiialika Toto Africans kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, kadhalika Ruvu shooting ikichea na Azam FC kwenye Uwanja wa Mabatini, Pwani.

Jumapili, Mwadui FC itacheza Mbeya City kwenye Uwanja wa Mwadui wakati African Lyon itacheza na Mtibwa Sugar Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam ilihali JKT Ruvu itakuwa mwenyeji wa Mbao FC kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga. Kwa ufupi, ratiba ya kesho iko kama ifuatavyo:   

11.02.2017 - STAND UNITED VS MAJIMAJI

11.02.2017 - SIMBA VS TANZANIA PRISONS

11.02.2017 - NDANDA FC VS TOTO AFRICAN

11.02.2017 - RUVU SHOOTING VS AZAM FC

12.02.2017 - MWADUI VS MBEYA CITY

12.02.2017 - AFRICAN LYON VS MTIBWA SUGAR

12.02.2017 - JKT RUVU VS MBAO FC

Kwa upande wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL), Kundi A mechi zinatarajiwa kupigwa leo Februari 10, mwaka huu ambako Lipuli itaikaribisha Ashanti United kwenye Uwanja wa Samora mjini Iringa wakati Pamba itacheza na Mshikamano ilihali Friends rangers itacheza na Kilivya United wakati Polisi Dar itapambana na Africans Sports.

10.02.2017 - LIPULI VS ASHANTI

10.02.2017 - PAMBA VS MSHIKAMANO

10.02.2017 - FRIENDS RANGERS VS KILUVYA

10.02.2017 - POLISI DAR VS AFRICAN SPORTS

Kundi B

Kundi B kesho Jumamosi Februari 11, mwaka huu itacheza na Mlale JKT kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea wakati Njombe Mji itacheza na Coastal Union kwenye Uwanja wa Makambako mkoani Njombe.

11.02.2017 - MLALE JKT VS KURUGENZI FC

11.02.2017 - NJOMBE MJI VS COASTAL UNION

Kundi C

Kundi C kutakuwa na mechi nne ambako Mgambo Shooting itacheza na Polisi Dodoma wakati Polisi Mara itakuwa mwenyeji wa Mvuvumwa ya Kigoma wakati Rhino Rangers itakuwa mgeni wa Panone huko Kilimanjrao na Singida United itacheza na Alliance mjini Singida.

11.02.2017 - MGAMBO SHOOTING VS POLISI DODOMA

11.02.2017 - POLISI MARA VS MVUVUMWA

11.02.2017 - PANONE VS RHINO RANGERS

11.02.2017 - SINGIDA UNITED VS ALLIANCE SCHOOL

Ligi Daraja la Pili leo Februari 10, kutakuwa na mchezo mmoja wa Kundi A kati ya Mirambo ya Tabora na Bulyanhulu ya Shinyanga wakati Jumapili Februari 12, mwaka huu kutakuwa na mechi tatu ambazo ni za Kundi D.

Mechi nyingine ni kati ya Namungo na Mawenzi; Sabasaba na The Mighty Elephant wakati Mkamba Rangers itacheza na Mbalali United.

10.02.2017 - MIRAMBO VS BULYANHULU

12.02.2017 - NAMUNGO VS MAWENZI

12.02.2017 - SABASABA VS THE MIGHTY ELEPHANT

12.02.2017 - MKAMBA RANGERS VS MBARALI UNITED