Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, February 28, 2017

Diamond, Kiba Uso kwa Uso, Kamati ya Serengeti Boys

WAZIRI wa habari sanaa utamaduni na michezo Nape Nnauye amewateua wanamuziki wa kizazi kipya Diamond Platinum na Ally Kiba kuwemo kwenye kamati ya watu 10 ya uchangishaji pesa kwa ajili ya timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ‘Serengeti Boys’ itakayoshiriki michuano ya Afrika nchini Gabon mwezi Mei.
Kamati hiyo iliyogusa sekta mbalimbali itakuwa chini ya mwenyekiti Charles Hillary na katibu Selestine Mwesigwa huku wajumbe pamoja na Diamond na Kiba wapo Beatrice Singano, Ruge Mutahaba, Eric Shigongo, Maulidi Kitenge, Hoyce Temu na Hassan Abas.

Waziri Nape alisema majukumu ya kamati hiyo ni kuhamasisha wadau mbalimbali kuichangia Serengeti ambayo itaiwakilisha nchi kwenye michuano ya vijana Afrika ili kuhakikisha inafanya vizuri na kuipeperusha vema bendera ya Taifa.
“Nina imani na timu hii kwani imegusa kila mahali kuanzia Serikalini, TFF, Burudani na katika vyombo vya Habari ili kuhakisha kila Mtanzania anachangia ili vijana hawa waweze kufanya vizuri”, alisema Nape.
Akizungumzia michuano ya Olimpiki itakayofanyika Tokyo Japan mwaka 2020 Waziri Nape alisema “Tumejipanga katika Olimpiki ya Tokyo 2020 kupeleka timu ya soka na itakuwa mara ya kwanza katika historia ya nchi na tunataka kwenda kushindana na si kushiriki”.