Rafiki wa karibu wa Juuko alisema kuwa beki huyo alitua majira ya saa sita usiku baada ya kumaliza matatizo yake ya kifamilia ikiwemo kufiwa na watoto wake watatu wakati yeye akiwa na timu ya taifa ya Uganda iliyoshiriki fainali za AFCON.
Mara kadhaa viongozi wa Simba walipokuwa wakimtafuta beki huyo ili arejee na kujiunga na kikosi chao mawasiliano baina yao yalikuwa magumu ingawa baadaye aliwasiliana nao na kuwaambia anasubiri tiketi kutoka Shirikisho la Soka la Uganda (FUFA).
Aveva alithibisha ujio wa ‘mkoba’ huo ndipo alipokiri na kubainisha kuwa wanamkabidhi mikononi mwa Omog ili aamue mwenyewe kama kumtumia au la.
“Niliwasiliana naye jana akiwa Uwanja wa Ndege huko kwao wakati anajiandaa kuja Dar es Salaam, hivyo hizo taarifa ni kweli na anapaswa kujiunga na wenzake ingawa leo wamepewa mapumziko.
“Juuko ni mchezaji wetu kwasababu ana mkataba na Simba utakaomalizika Disemba hivyo ilikuwa ni lazima aje ajiunge na timu ili mambo mengine yaendelee kama anataka kwenda kucheza sehemu nyingine, tukae na kuzungumza. Kocha Joseph Omog ndiye atajuwa jinsi ya kumtumia hilo ni jukumu lake na tunamwachia,” alisema Aveva.
Tangu kuondoka kwake Abdi Banda amekuwa akicheza nafasi hiyo pamoja na Method Mwanjali ingawa mechi ya jana ambayo walishinda mabao 2-1 dhidi ya Yanga alipangwa Novaty Lufunga kutokana na Mwanjali kuwa majeruhi.
No comments:
Post a Comment