Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, January 20, 2017

Nape apongeza Uzalendo wa Multichoice Tanzania kwa kumsapoti Alphonce Simbu

Waziri wa Habari, utamaduni, michezo na Sanaa Mh. Nape Nnauye amepongeza juhudi zinazofanywa na Kampuni ya Multichoice Tanzania   na kuonesha uzalendo wa kusaidia michezo ikiwemo kumsaidia Mwanariadha Alphonce Alex Simbu ambaye amedizi kung’ara kwa sasa kwa upande wa riadha.
Waziri Nape ameyasema hayo mapema leo Jijini Dar es Salaam wakati wa kumpokea  rasmi mwanariadha huyo tokea aliporejea kushiriki michuano mikubwa ya mbio za 14 za Standard Chartered Mumbai Marathon, nchini India na kuibuka shujaa zilizomalizika hivi karibuni.
“Serikali inajivunia kuwa na vijana wanailetea heshima Tanzania. Uzalendo wako Simbu ni chachu ya kwa vijana wengine kwani nao matamanio yao ni kushinda kama ulivyoshinda wewe tunakupongeza sana. Pia tunaipongeza Multichoice Tanzania kwa Uzalendo wa kuchukua jukumju la kumsimamia Simbu kwa muda wa mwaka mmoja, Tunataka na wadau wengine waige mfano kama huu wa Multichoice Tanzania kwani ni wa kizalenod” ameeleza Waziri Nape.
Na kuongeza kuwa, kuna mamlaka zingine zinatumia mabilioni ya pesa kupeleka kudhamini mambo mengine na kuacha vijana wenye kupeperusha bendera ya Tanzania nje ya Tanzania huku pesa hizo zikiteketea bure” amebainisha Waziri Nape.
Kwa upande wake, Simbu ameshukuru Serikali, wadau ikiwemo Multichoice, Wanahabari,familia yake na viongozi wa mchezo wa raidha hapa nchini kwa kumpa sapoti kwa kila anachokifanya kwani ameongeza juhudi na hali ambayo inamfanya aweze kufikia ushindi huo anaoupata kwa sasa.Waziri wa Habari, utamaduni, michezo na Sanaa Mh. Nape Nnauye akisalimiana na mwanariadha Alphonce Simbu wakati wa tukio hilo.

Waziri wa Habari, utamaduni, michezo na Sanaa Mh. Nape Nnauye akiingia katika mkutano huo wa utambulisho 

Waziri wa Habari, utamaduni, michezo na Sanaa Mh. Nape Nnauye akiwa na Mwanariadha Alphonce Simbu wakati wa tukio hilo
Mwanariadha Alphonce Simbu akielezea namna alivyoweza kuonesha maajabu yake na kuibuka

Waziri Nape akizungumza katika tukio ambapo amewataka wadau kama Dstv kuendelea kujitokeza kusaidia vipaji vya vijana hapa nchini 


Waziri Nape akimvisha Mwanaraidha Simbu medali yake aliyoshinda huko India, kuonyesha ishara ya kumpokea na kutambua mchango wake


Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo akipiga picha  ya pamoja na Simbu pamoja na zawadi zake alizoshinda nchini India.

Simbu akiwa na Medali yake

Simbu akionesha ushindi wake huo

Simbu akipiga picha ya pamoja na viongozi wa RT