Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, January 24, 2017

TFF YAFUNGA UWANJA WA JAMHURI MOROGORO NA KICHANGANI WA LIPULI



SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imesimamishwa Uwanja wa Jamhuri Morogoro kutumika ili kutoa fursa kwa wamiliki kufanya marekebisho makubwa kwenye eneo la kuchezea.
Akizungumza na wandishi wa habari jana, Ofisa habari wa TFF, Alfred Lucas alisema hatua hiyo imefikiwa baada ya mchezo wa Mtibwa Sugar dhidi ya Simba kuonekana sehemu ya kuchezea ikiwa kwenye hali mbaya hivyo inahitaji marekebisho.
"Tumesimamisha matumizi ya uwanja wa Jamhuri kupisha marekebisho endapo hayatafanyika, uwanja huo hautatumika pia JKT Ruvu wameomba kuhama kutoka Mabatini kwenda Uwanja wa Mkwakwani Tanga," alisema Lucas.
Pia uwanja wa Kichangani umeondolewa kutumika kwa mechi za ligi, hivyo klabu za Iringa sasa timu zao zitatumia Uwanja wa Kumbukumbu ya Samora mjini humo kwa mechi zao la ligi.
Lucas alisema baada ya mchezo kumalizika mashabiki waliingia uwanjani kwa wingi na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wachezaji, waamuzi na waandishi wa habari hali ambayo ilisababisha kamera ya Azam Tv kuangushwa na washabiki hao.
Pia Lucas alisema JKT Ruvu imeomba kubadilisha uwanja wake wa nyumbani kutoka Mabatini Pwani kwenda Mkwakwani Tanga kutokana na wachezaji wake 12 kwenda kwenye mafunzo ya kijeshi mkoani Tanga.
"Ombi hilo limekubaliwa kwa mujibu wa Kanuni ya 6(6) ya Ligi Kuu, TFF/TPLB zina mamlaka ya mwisho kuhamisha kituo cha mchezo kwa sababu inazoona zinafaa na kwa wakati husika," alisema Lucas.
TFF imewataka askari polisi kuwa makini katika majukumu yao ya kusimamia usalama uwanjani na kuacha kutumia nguvu kubwa katika kudhibiti fujo kwa wachezaji uwanjani.

No comments:

Post a Comment