Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, January 8, 2017

MADJ WA AFRIKA KUSINI WASEMA MUZIKI WA BONGO UNAKUWA 
MA DJ Siyabonga Sibeko ‘DJ Capital’ na Lutendo Kungoane ‘Dj Sliqe’ toka Afrika Kusini wamesema wasanii Diamond na Vanessa Mdee ndio wasanii wa Tanzania wanaowavutia kwa sasa.
Madj hao ambao wapo nchini kwa ziara ya wiki moja kujifunza muziki wa Tanzania wamesema muziki wa Tanzania utafika mbali kama wasanii watajituma zaidi na kuutangaza kimataifa.
Wakizungumza Dar esSalaam madj hao kutoka  redio na  vituo vya luninga, Afrika Kusini walisema Tanzania imepiga hatua kubwa kimuziki katika nchi za Afrika zinazofanya vizuri ikiongozwa na Afrika Kusini, Nigeria, Ghana na Kenya.
 “Huwezi kuzungumzia nchi zinazofanya vizuri kimuziki kwa kiwango cha juu Afrika bila kutaja Tanzanja hivyo tumekuja kujifunza na kukutana na wasanii kwa sababu pia sisi ni watayarishaji wa muziki,”alisema Dj Capital.
Naye DJ Sliqe alisema anavutiwa na Diaamond na Vanessa Mdee japo Tanzania kuna  wasanii wengi wanaofanya vizuri kwa sasa, lakini kwa  upande wake anawapenda zaidi hao
Wote ni Ma DJ wa kituo cha Radio cha Touch Central cha Johannesburg, Afrika Kusini wakati DJ Capital pia anafanya kipindi cha Club 808 cha Televisheni ya ETV ya nchini lakini pia wanapiga muziki madj kwenye kumbi za starehe.