Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, December 19, 2016

TEVEZ AWABWAGA MESSI, RONALDO KWA MSHAHARA ANAOLIPWA CHINASIKU chache zijazo Mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina, Carlos Arberto Martinez Tevez,atakuwa tajiri mkubwa na mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi duniani hii ni baada ya kuripotiwa kuwa yuko karibu kabisa kusaini mkataba wa miaka miwili wa kujiunga na matajiri wa China klabu ya Shanghai Shenhua.


Ishu iko hivi Tevez,32,aliyewahi kutamba na vilabu vya Manchester United,Manchester City na Juventus amepata dili la kujiunga na Shanghai Shenhua.


Dili hilo litamfanya Tevez awe akilipwa mshahara wa Paundi 615,000 kwa wiki na hivyo kuwa mchezji anayelipwa zaidi duniani tena ziadi ya Cristiano Ronaldo anayelipwa £365,0000 na Lionel Messi anayelipwa 266,368.


Huu ndiyo mchanganuo wa mshahara wa Tevez


Mwaka:£31,980,000

Siku:£87,857

Saa:£3,660.71.

Dakika:£61.01

Sekunde:£1

Michezo 30 kwa msimu:£11,581