Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, December 9, 2015

FA yamfungia michezo mitatu Schweinsteiger

Manchester-United-Man-United-News-Man-United-Transfers-Transfer-News-Bastian-Schweinsteiger-Schweinsteiger-Man-United-Man-597414Chama cha Soka cha Engaland (FA) kimemfungia kiungo wa Manchester United, Bastian Schweinsteiger (pichani) kwa michezo mitatu baada ya kumchezea vibaya mchezaji wa West Ham United, Winston Reid
Katika taarifa ya FA inasema Schweinsteiger alifanya kosa hilo katika mchezo wa jumamosi wakati timu hizo zilipokutana na kutoka sare ya bila kufungana.
FA ilisema Schweinsteiger alimpiga kwa kiwiko Reid wakati wakigombea mpira na refa wa mchezo huo, Mark Clattenburg hakuona tukio hilo lakini baada ya FA kupitia video ya mchezo walimkuta Schweinsteiger kuwa na hatia na kumfungia michezo mitatu.
Hata hivyo pamoja na adhabu ambayo amepewa Schweinsteiger lakini pia ana nafasi ya kukata rufaa ambapo mwisho wa kupokea rufaa hiyo ni Disemba 10.
Baada ya kifungo hicho Schweinsteiger atakosa michezo ya Bournemouth, Norwich na Stoke City na atarejea katika mchezo wa Chelsea Disemba 28.