Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, December 19, 2016

RAHEEM STERLING APELEKA KILIO EMIRATES


Manchester City Leo huko kwao Etihad wametoka nyuma kwa Bao 1-0 na kuitandika Arsenal 2-1 katika Mechi ya EPL, Ligi Kuu England.
Hiki ni kipigo cha Pili mfululizo kwenye EPL kwa Arsenal baada ya Majuzi kupigwa 2-1 huko Goodison Park mikononi mwa Everton.
Sasa Arsenal wameporomoka hadi Nafasi ya 4 wakiwa nyuma ya Liverpool, Man City na Vinara Chelsea.
Hii Leo, Arsenal walitangulia kufunga katika Dakika ya 5 kwa Bao la Theo Walcott ambalo lilidumu hadi Haftaimu.

Kipindi cha Pili Man City walikuja wapya na kuirudisha Arsenal nyuma na Dakika ya 47 kusawazisha kwa Bao la Leroy Sane.
Bao la ushindi kwa City lilifungwa Dakika ya 71 na Raheem Sterling huku David Silva akionekana kuwa Ofsaidi akimkaribia Kipa Petr Cech na hilo bila shaka litawafanya Arsenal kulalamikia Bao hilo.

Kwenye Mechi nyingine za EPL hii Leo, Tottenham iliichapa Burnley 2-1 na mapema Southampton kuibomoa Bournemouth 3-1.
Kesho Jumatatu Usiku ipo Mechi moja Usiku huko Goodison Park kati ya Everton na Liverpool ikiwa ni Dabi ya Merseyside.