KOCHA Mkuu
wa timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 'Serengeti Boys' Bakari
Shime amekabidhiwa mikoba ya kuinoa JKT Ruvu kuanzia mzunguko wa pili wa ligi kuu
utakaoanza Disemba 17.
Shime anachukua nafasi ya kocha Malale Hamsini
ambaye alianza kuifundisha timu hiyo mwanzoni mwa msimu huu akitokea Ndanda FC.
Akizungumza
na gazeti hili Ofisa Habari wa JKT Ruvu, Constantine Masanja alisema uongozi umeamua
kufanya marekebisho kwenye benchi la ufundi ili kuhakikisha wanafanya vizuri
baada ya mzunguko wa kwanza kumaliza wakiwa nafasi ya 14 huku wakiwa na pointi 13."Uongozi umefanya mabadiliko kwenye benchi la ufundi sasa kocha mkuu ni Shime akisaidiwa na Mwamgaya pamoja na Sajini Abdallah," alisema Masanja.
Masanja alisema usajili uongozi umemuachia kocha Shime kuamua kupunguza au kuongeza wachezaji kabla ya kufungwa dirisha la usajili, Disemba 15
Ruvu wameingia kambini Novemba 25 kujiandaa na mikikimikiki ya duru la pili kwenye Uwanja wa JKT Mbweni chini ya kocha huyo wa zamani wa Mgambo JKT ya Tanga ambayo sasa inashiriki Ligi Daraja la Kwanza.
No comments:
Post a Comment