Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, December 1, 2016

EL CLASICO JUMAMOSI, CRISTIANO RONALDO NJE KUIVUTIA KASI MECHI YAO NA BARCA


KOCHA wa Real Madrid Zinedine Zidane alimpumzisha Cristiano Ronaldo ya jana ya Real Madrid ya Copa del Rey dhidi ya Cultural Leonesa ili kuhakikisha anakuwa fiti kwa Asilimia 100 kwa El Clasico ya Jumamosi hii huko Nou Camp na Barcelona.
Mechi hiyo ya Jumamosi mbali ya kuwa ni El Clasico ni nafasi murua kwa Real, ambao wanaongoza La Liga wakiwa Pointi 6 mbele ya Timu ya Pili Barca, kufungua pengo na Mahasimu hao kuwa Pointi 9.

Katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Timu 32 ya Copa del Rey walipocheza Ugenini na Cultural Leonesa, Real walicheza bila ya Ronaldo na kushinda 7-1 kwa Bao za Gianni Zuiverloon, alijifunga mwenyewe, Marco Asensio, Bao 2, Alvaro Morata, Bao 2, Nacho Fernandez na Mariano Diaz.
Lakini Zidane amesema Kiungo wa Brazil, Casemiro, atacheza Mechi hiyo itakayochezwa Santiago Bernabeu baada ya kuwa nje kwa Miezi Miwili baada ya kuvunjika Mfupa wa Mguuni.

Wakati hii itakuwa ni Mechi ya Pili ya Raundi ya Mtoano ya Copa del Rey kwa Real, Timu nyingine kuanzia Leo zitakuwa zikicheza Mechi zao za Kwanza za Raundi hii na kurudiana Desemba 21.

Hilo ni kwa sababu Real wanapaswa kusafiri kwenda Japan kuanzia Desemba 8 ili kucheza Mashindano ya FIFA ya Kombe la Dunia kwa Klabu wao wakiwakilisha Bara la Ulaya kwa vile ni Mabingwa wa Ulaya.

Alhamisi, FC Barcelona watacheza Mechi yao ya Kwanza ya Raundi ya Timu 32 ya Copa del Rey Ugenini huko Estadio Jose Rico Perez na Hercules CF.

COPA DEL REY
Raundi ya Timu 32
Jumanne Novemba 29

22:00 CD Leganes v Valencia C.F
23:00 Sporting Gijon v SD Eibar
23:00 Alcorcon v RCD Espanyol

Jumatano Novemba 30
0:00 Real Betis v Deportivo La Coruna
21:00 CD Toledo v Villarreal CF
21:00 Formentera v Sevilla FC
23:00 Real Madrid CF v Cultural Leonesa [Mechi ya Kwanza, 7-1]
23:00 Cordoba CF v Malaga CF
23:00 Granada CF v Osasuna
23:00 UCAM Murcia v Celta de Vigo
23:00 Guijuelo v Atletico de Madrid

Alhamisi Desemba 1
0:00 Hercules CF v FC Barcelona
22:00 Real Valladolid v Real Sociedad
23:00 Gimnastica v Deportivo Alaves
23:00 Huesca v Las Palmas

Ijumaa Desemba 2
0:00 Real Racing Santander v Athletic de Bilbao