Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, November 14, 2016

NAPE ATOA NENO KUHUSU UREMBO




WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amesema serikali ya awamu ya tano itahakikisha mashindano ya ulimbwende yanakuwa na thamani na yenye faida.
Nape aliyasema hayo wakati akimkabidhi bendera ya Taifa, Miss Ilala 2016, Julitha Kabete ambaye pia ni mshiriki wa mashindano ya Miss Tanzania 2016, ambaye anakwenda kushiriki mashindano ya urembo Afrika yatakayofanyika Novemba 26 katika kitongoji cha Calabar kilichopo Nigeria.
“Tunataka mashindano ya Miss Tanzania ambaye anafaidika sio mshindi peke yake tumeona hapa huyu alikuwa mshindi wa nne na amepata nafasi ya kuwakilisha nchi, tunafahamu mashindano ya Miss Tanzania yalikuwa yamefungiwa kufanyika ila sasa yamerudi vizuri,  tutaendelea kuyaimarisha yawe bora na matarajio ya serikali ni kuona tunakuwa tunafanya vizuri na siku moja hata mshindi wa Miss World atoke Tanzania,” alisema Nape.
Pia Nape alisema serikali inamtakia safari njema na ipo nyuma yake kumpa msaada pindi unapohitajika.
Akizungumza wakati wa kukabidhiwa Miss Julitha Kabete amesema amejiandaa kwa ajili ya mashindano hayo na anaamini atafanya vizuri kwenye mashindano hayo ambayo ndio kwanza yaanza
 “Naomba Watazania wanisapoti ili nifanikiwe kushinda Miss Africa ambayo inafanyika Nigeria, ni nafasi ya kipekee ambayo nimepata na nikipata ushindi ni wetu sote,” alisema Julitha.
Mashindano hayo yatafanyika kwa mara ya kwanza Afrika nayatafanyika katika kitongoji cha Calabar kilichopo Nigeria.

No comments:

Post a Comment