Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, August 6, 2016

SERENGETI BOYS KIBARUANI LEO AFRIKA KUSINI
TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ‘Serengeti Boys’, leo inashuka dimbani kumenyana na wenyeji Afrika Kusini katika Uwanja wa Dobsonville ulioko Soweto, kwenye  mchezo wa kuwania nafasi ya kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, zitakazofanyika Madagascar mwakani.

Kocha Mkuu wa Serengeti boys,  Bakari Shime amejigamba kuwa wataibuka na ushindi katika mchezo huo kwa sababu vijana wake wamekuwa wakifanya kile anachowafundisha.
 “Tutaifunga Afrika Kusini hapa kwao hilo linawezekana japokuwa hata wao wamejipanga tutajitahidi kutumia nafasi tutakazopata ili mechi ya marudiano iwe nyepesi kwetu” alisema Shime.

Mchezo huo utakaoanza saa 9.00 alasiri kwa saa za Afrika Kusini wakati huku Tanzania itakuwa ni saa 10.00 jioni katika uwanja ambao hutumiwa na timu ya Moroka Swallows ambayo kwa sasa imeshuka daraja hadi la pili.
Baadaya mchezo huu timu hizi zitarudiana Agosti 21 katika Uwanja wa Azam ulioko Chamazi-nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Endapo Serengeti boys itafanikiwa kuitoa Afrika Kusini itakutana na msindi kati ya Congo Brazaville na Namibia.