Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, August 6, 2016

MANJI AWAVUA UANACHAMA WAJUMBE WATATU WA KAMATI YA UTENDAJIWANACHAMA wa klabu ya Yanga wamewavua uanachama wajumbe watatu wa kamati ya Utendaji baada ya kile kinachosadikika kuwa ni usaliti wanaoufanya.

Wajumbe hao ni Ayubu Nyenzi,Hashim Abdallah na Salumu Mkemi ambaye siku mbili zilizopita alisikika katika radio ya EFM akizungumza kuwa mkutano huu mkuu ni batili kutokana na kukiukwa kwa katiba ya Yanga.

Naye mjumbe Hashimu Abdallah ambaye alikuwepo katika ukumbi ameondoka muda mfupi baada ya kuvuliwa uanachama huku akigoma kuongea na waandishi wa habari huku akisema atapanga siku maalum ya kuongea nao.

"Siongei chochote mpaka muda ukifika nitawaita nitazungumza nanyi lakini sio leo"alisema Hashim.

Wakati huo huo Mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuph Manji amemsamehe mjumbe Siza Lyimo ambaye aliomba radhi mbele ya wanachama baada nae kuonekana kuwa ni msaliti.