KATIBU Mkuu
wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) Selestine Mwesigwa amewaasa makocha wa
magolikipa kuitumia vema taaluma waliyoipata.
Mwesigwa
alitoa rai hiyo wakati akifunga kozi ya juu ya makocha wa magolikipa iliyokuwa
inaendeshwa na mkufunzi wa Fifa, Alejandro Heredia.
“Mpira ni
golikipa hivyo taaluma yenu ni muhimu sana kwa mustakabali wa soka la Tanzania
hivyo mkawe chachu ya soka mkishirikiana ninyi kwa ninyi”, alisema Mwesigwa.
Pia Mwesigwa
alisema kama mwenzenu atahitaji msaada msaidiane na siyo kukaa kimya wakati
timu yake ikifanya vibaya.
Naye
Mkufunzi Heredia aliwashukuru makocha hao kwa ushirikiano waliompa kwani
wamefanya kazi yake kuwa rahisi na anaamini watakuwa makocha bora wa makipa.
Kozi hiyo ya
siku saba ilikuwa na washiriki 26 toka kwenye timu za ligi kuu Tanzania Bara na
timu za Taifa.
No comments:
Post a Comment