Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, July 28, 2016

SAHARA MEDIA KUONESHA MAPAMBANO YA NGUMI LIVE
KAMPUNI ya Hall of Fame boxing and Promotions kwa kushirikiana na kampuni ya Sahara media group wameingia mkataba wa miaka mitatu wa kuonesha mapambano ya ngumi live.
Akizungumza na wandishi wa habari juzi, Mkurugenzi wa vipindi wa Sahara media,  Yusuph Kamote alisema lengo la makubaliano hayo ni kuinua na kutangaza mchezo wa ngumi ili kuongeza kipato kwa mabondia wazawa.
"Umahiri wa Kampuni ya Hall of fame boxing and Promotions katika kuinua ndondi na mikakati iliyopo katika kuandaa mapambano ndio umetuvutia kuingia nao mkataba" alisema Kamote
Naye Mkurugenzi wa Hall of fame boxing and Promotions Jay Msangi alisema pambano la kwanza ambalo litaanza kuonesha  litafanyika Agosti na mashabiki wa ndondi wa mikoani watapata fursa ya kuona live.
"Mara nyingi ngumi zinachezwa Dar es Salaam na kuwanyima fursa watu wa mikoani lakini kutokana na haya makubaliano na star tv itawapa fursa ya kufuatilia moja kwa moja",   alisema Msangi. 
Hii ni fursa pekee kwa mabondia kuonyesha uhodari wao ndani na nje pamoja na kujipatia kipato.