MFANYABIASHARA maarufu nchini, Mohammed
Gulam Dewji ama 'MO' amesema yupo tayari kufanya uwekezaji wa bilioni 20, Simba
endapo tu wanachama wa klabu hiyo wataridhia mpango wake.
Mo amekuwa akihusishwa kutaka
kufanya uwekezaji mkubwa ndani ya Simba huku baadhi ya wanachama wa klabu hiyo
wakionekana kutokuwa tayari kutokana na sababu zao binafsi.
Akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake, Dar es Salaam leo MO amesema kinachomvutia kufanya uwekezaji huo
mkubwa kwa Simba ni mapenzi aliyonayo kwa klabu hiyo.
"Naipenda Simba toka moyoni,niliwahi
kuidhamini miaka ya nyuma na tulifanya vizuri sana katika michuano ya kimataifa
kila mwanasimba analijua," amesema MO.
Wakati huohuo Mo amesema bajeti
ndogo ya Simba ndiyo inayoifanya klabu hiyo kushindwa kushindana vizuri katika
soko la usajili na klabu za Yanga na Azam.
Mo ameongeza kuwa endapo atapewa
ridhaa ya kufanya uwekezaji basi ndani ya miaka mitatu ataijengea klabu hiyo
kiwanja bora cha mpira, hosteli, Gym na kuajiri makocha wenye vigezo.
Simba inatarajiwa kufanya mkutano
mkuu wa wanachama utakaojadili juu ya uendeshwaji wa klabu hiyo siku ya
Jumapili katika Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay
No comments:
Post a Comment