Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, July 29, 2016

DILI YA PAUL POGBA KWENDA MAN UNITED YAIVA


RIPOTI zimevuja kuwa Manchester United wamefikia hatua nzuri katika Dili yao na Mabingwa wa Italy Juventus na sasa watakamilisha Uhamisho wa Dau la Rekodi ya Dunia kwa kumnunua Kiungo Paul Pogba ndani ya Masaa 48.
FILE PHOTO: The agent of Paul Pogba has stated his client is not desperate to leave Turin, following speculation linking him with a move to Manchester United Paul Pogba, Manchester United ... Soccer - Barclays Premier League - Manchester United v Stoke City - Old Trafford ... 31-01-2012 ... Manchester ... United Kingdom ... Photo credit should read: Neal Simpson/EMPICS Sport. Unique Reference No. 12678348 ...Ripoti hizo zimedai Man United wametoa Ofa mpya ya Euro Milioni 110 na Euro Milioni 10 juu ikiwa ni nyongeza mbalimbali [Jumla Pauni Milioni 100] huku Juve waking’ang’ania kupewa Euro Milioni 5 ya ziada endapo Pogba ataongeza Mkataba na Man United.
Pia kile kikwazo cha Wakala wa Pogba, Mino Raiola, cha kutaka kulipwa Mgao wa Euro Milioni 20 kutoka kwenye Ada ya Uhamisho ambazo Juve walitaka Man United walipe zote na si kukatwa kwenye Dau lenyewe sasa inaelekea kimekwisha kwa maelewano kati ya Raiola na Man United.

Kukamilika kwa Dili hii kutaleta afueni kubwa kwa Juve kwani Juzi waligongwa Euro Milioni 90 walipomnunua Straika wa Argentina, Gonzalo Higuaín, kutoka Napoli.
Pogba aliondoka Man United Mwaka 2012 bila Ada ya Uhamisho baada ya kugomea Mkataba mpya na Man United ikaambua Pauni 800,000 tu kama Fidia ya kukuza kipaji chake.
Akiwa na Juve, Pogba alipanda chati na kuwa nguzo kubwa ya Juve akiwabeba kutwaa Ubingwa wa Serie A kila Mwaka katika Miaka yake yote Minne.
Dau la Uhamisho la Pogba litavunja zile Rekodi za Dunia za kuhamia Real Madrid za Gareth Bale, toka Tottenham kwa Pauni Milioni 85, na Cristiano Ronaldo toka Man United kwa Pauni Milioni 80.

Akitua Old Trafford, Pogba atakuwa Mchezaji wa 4 mkubwa kununuliwa na Meneja Mpya Jose Mourinho katika kipindi hiki.
Wengine ni Zlatan Ibrahimovic, Eric Bailly na Henrikh Mkhitaryan.
Pogba’s agent Mino Raiola is negotiating with Manchester United