Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, February 23, 2016

UEFA CHAMPIONS LEAGUE, LEO NI ARSENAL vs BARCELONA, JUVENTUS vs BAYERN MUNICH

LEO Usiku Arsenal wana kimbembe kikubwa Uwanjani kwao Emirates watakapocheza Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONS LIGI, UCL, dhidi ya Mabingwa Watetezi FC Barcelona.
Lakini Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger anategemea Kipa wake Petr Cech ataendeleza rekodi yake ya kutowahi kufungwa Goli na Lionel Messi.

Katika Mechi 8 akiwa Kipa wa Chelsea, Cech hajafungwa na Messi na Miaka Minne iliyopita alisaidia kuibwaga Barca kwenye Nusu Fainali ya UCL na pia kuwahi kuokoa Penati ya Messi wakati Chelsea waliposhinda na kutinga Fainali ambako walitwaa Kombe.

Wenger amejiliwaza kwa kusema: “Natumai Cech atatupa moyo mkubwa na atamtuliza Messi. Natumai Messi ataweweseka na historia kuwa upande wetu!”
Hata hivyo Barca ya sasa si Messi peke yake kwani Mashambulizi yao ni ya Mtu 3 wakiwepo pia Luis Suarez na Neymar.
DONDOO:
-Barcelona na Real Madrid ndio pekee hazijafungwa kwenye UCL Msimu huu.
Hii ni mara ya 3 kwa Arsenal kukutana na Barca kwenye hatua hii ya Mashindano haya na mara zote mbili za, Mwaka 2010 na 2011, walibwagwa nje ingawa 2011 walishinda Mechi ya Kwanza Bao 2-1 kwa Bao za Robin van Persie na Andrei Arshavin.
Arsenal, ambao Miaka 10 iliyopita walibwagwa 2-1 na Barca kwenye Fainali ya UCL ambayo Kipa wao Jens Lehmann alitolewa nje kwa Kadi Nyekundu mapema kwenye Fainali hiyo, wanajipa sana moyo pale Meneja wao Wenger alipoeleza: “Barca ndio ‘Washindi Watarajiwa’ hivyo inabidi sisi tucheze Gemu ya juu kabisa. Lazima tuwe na mkazo. Tujiamini na tujitume!”

MTANANGE HUU WA LEO USIKU
Arsenal, ambao walimaliza Nafasi ya Pili kwenye Kundi F nyuma ya Bayern Munich, ndio Timu pekee pamoja na Real Madrid kuingia Hatua za Mtoano za UCL kila Msimu tangu Mashindano haya yatumie Mfumo mpya kuanzia Msimu wa 2003/04.
Lakini katika Misimu Mitano iliyopita, Arsenal wamekuwa wakitupwa nje kwenye hatua hii.
Barcelona, waliomaliza Washindi wa Kundi E mbele ya AS Roma, wamekuwa wakitinga Hatua za Mtoano za UCL kwa Misimu 12 hadi sasa na wamefika Nusu Fainali mara 7 kati ya 8 zilizopita.
Mara pekee ambayo walitolewa Robo Fainali katika kipindi hicho ni Msimu wa 2013/14 walipobwagwa na Atletico Madrid. Katika Misimu 10 iliyopita, Barca wametwaa Ubingwa wa Ulaya mara 4.
UEFA CHAMPIONS LIGI
RAUNDI YA MTOANO YA TIMU 16
JUMANNE 23 FEB 2016
Mechi kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku

Arsenal vs Barcelona
Juventus vs Bayern Munich

No comments:

Post a Comment