Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, February 23, 2016

UNITED, CHRIS SMALLING, JUAN MATA NA LINGARD WAIPELEKA ROBO FAINALI UNITED


Ndani ya Uwanja wa Greenhous Meadow, Manchester United waliisambaratisha Timu ya Daraja la chini la Ligi 1, Shrewsbury Town, katika Mechi ya mwisho ya Raundi ya 5 ya EMIRATES FA CUP Bao 3-0 na kutinga Raundi ya 6 ambayo ni Robo Fainali ambapo watakutana na West Ham huko Old Trafford.
Bao za Kipindi cha Kwanza za Dakika za 37 kupitia Chris Smalling na Frikiki ya Juan Mata ya Dakika ya 45 ziliwapa Man United uongozi wa 2-0 hadi Mapumziko.
Jesse Lingard alipiga Bao la 3 Dakika ya 61 na kuwapa Man United ushindi wa raha wa 3-0 ambao umeondoa presha kwa Meneja wao, Luis van Gaal, anaesakamwa hasa baada ya kufungwa Mechi 2 mfululizo zilizopita dhidi ya Sunderland, kwenye Ligi Kuu England, na toka kwa FC Midtjylland huko Denmark kwenye UEFA EUROPA LIGI.
Alhamisi, Man United wako kwao Old Trafford kurudiana na FC Midtjylland wakitakiwa kupindua ushindi wa Wadenishi hao wa Bao 2-1.