Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, December 3, 2015

KENYA, NIGERIA, SOUTH AFRICA ZAJIUNGA CHAMA CHA LIGI DUNIANI.

Kenya, Nigeria na South Africa zimeungana na Ligi nyingine kubwa za Soka la Kulipa kuunda WAL, World Association of Leagues, Chama cha Ligi za Dunia, kufuatia Mkutano uliofanyika huko Paris.
Nchi hizo 3 za Afrika zimeungana na Ligi nyingine 18, zikiwemo Ligi kubwa za England, France na Spain, kuunda chombo hicho ambacho kitafanya kazi sambamba na FIFA.

Kwa mujibu wa Rais wa LFP, Ligi ya France, Frederic Thiriez, Chombo hiki kitaanza kazi zake rasmi Mwezi Januari na kitajumuisha zile Ligi ambazo zinaendeshwa huru na si na Vyama vya Soka vya Nchi.

Washiriki wa Mkutano huo wa Paris wamesema umuhimu wa WAL unatokana na ukweli kuwa Ligi ndizo hudhibiti Asilimia 90 ya Soka na wao wanataka kushiriki katika maamuzi yeyote ya Soka yanayofanywa na FIFA na pia kutoa msukumo kuiunda upya FIFA yenyewe ambayo sasa ipo kipindi cha mpito kufuatia skandali kubwa za rushwa.

Mkutano huo wa Paris pia ulihudhuriwa na Wagombea Wanne wa Urais wa FIFA ambao ni Tajiri wa Afrika Kusini, Tokyo Sexwale, Prince Ali bin Al Hussein wa Jordan, Mwanadiplomasia wa France, Jerome Champagne, na Mkuu wa Soka huko Asia, Sheikh Salman bin Ebrahim Al Khalifa.

Akiongelea kuhusu kuundwa kwa WAL, Mtendaji Mkuu wa Ligi Kuu Kenya, Jack Oguda, amesema mbali ya kujenga uhusiano mzuri kati ya Ligi mbalimbali, Nchi za Afrika zitanufaika kutokana na hatua zilizochukuliwa huko Paris.

Oguda alisema: “Fursa hii ni kubwa. Hebu fikiria Ligi kubwa Duniani zikikutana kurekebisha Ligi zao kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2022 huko Qatar. Mikutano ya kuundwa kwa chombo hiki ilitupa nafasi kuona changamoto za Ligi nyingine. Afrika haiwezi kuwa nyuma na ni lazima ishiriki kikamilifu katika Soka la Dunia.”