Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, February 20, 2016

RATIBA YA LEO EMIRATES FA CUP MABINGWA ARSENAL vs HULL CITY, CHELSEA vs MAN CITY, MAN UNITED JUMATATU DHIDI YA SHREWSBURY


WIKIENDI hii Ligi Kuu England haina Mechi na badala yake zipo Mechi za Raundi ya 5 za EMIRATES FA CUP.
FA CUP, Kombe kongwe Duniani ambalo sasa limeongezwa Jina na kuitwa EMIRATES FA CUP kutokana na udhamini wa Kampuni ya Ndege ya UAE, Emirates Airlines, itafungua dimba Jumamosi huko Uwanjani Emirates Jijini London wakati Mabingwa Watetezi Arsenal wakicheza na Timu ya Daraja la chini la Championship, Hull City.

Baadae Siku hiyo zitafuata Mechi 3 ambapo Reading watacheza na West Bromwich Albion, Watford kuivaa Leeds United na Bournemouth kucheza na Everton.
Jumapili zipo Mechi 3 ikianza ile ya Blackburn Rovers na West Ham na kufuata ile ya Tottenham na Crystal Palace.
Mechi za Jumapili zitakamilika kwa mtanange mkali huko Stamford Bridge kati ya Chelsea na Man City.
Mechi ya mwisho ya Raundi ya 5 ni Jumatatu Usiku kati ya Shrewsbury na Manchester United.

EMIRATES FA CUP
Raundi ya 5
Jumamosi Februari 20

15:45 Arsenal v Hull City
18:00 Reading v West Brom
18:00 Watford v Leeds
20:15 Bournemouth v Everton

Jumapili Februari 21
17:00 Blackburn v West Ham
18:00 Tottenham v Crystal Palace
19:00 Chelsea v Man City

Jumatatu Februari 22
22:45 Shrewsbury v Man United THE EMIRATES FA CUP 2015/16
TAREHE MUHIMU
Raundi ya 3


Ijumaa 9 Januari 2016
Raundi ya 4
Jumamosi 30 Januari 2016
Raundi ya 5


Jumamosi 20 Februari 2016
Raundi ya 6-Robo Fainali

Jumamosi 12 Machi 2016
Nusu Fainali
Jumamosi 23 Aprili 2016 & Jumapili 24 Aprili 2016
Fainali Jumamosi 21 Mei 2016

No comments:

Post a Comment