Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, December 11, 2015

SWANSEA CITY WAMTAKA RYAN GIGGS AWE MENEJA WAO

Swansea wameripotiwa kuwa na nia ya kumtaka Meneja Msaidizi wa Manchester United Ryan Giggs kuchukua nafasi ya Meneja iliyo wazi Klabuni kwao.
Juzi, Swansea walimtimua Meneja wao Garry Monk aliedumu Miezi 22 baada ya Msimu huu kushinda Mechi 1 tu kati ya 11.
Kwenye Listi ya Watu wanaoweza kuchukua nafasi hiyo ya Umeneja wa Swansea pia yupo Meneja wa zamani wa Swansea, Brendan Rodgers, ambae hivi karibuni alitimuliwa Liverpool na pia David Moyes, Meneja wa zamani wa Everton na Man United ambae Wiki chache zilizopita aliondolewa huko Spain Klabuni Real Sociedad.

Lakini Gazeti la Uingereza la The Independent linaamini Ryan Giggs yupo juu kwenye Listi ya Swansea ya Mtu anaewafaa.
Giggs amekuwa Masaidizi wa Meneja wa MaN United Louis van Gaal tangu Mdachi huyo apewe wadhifa huo Mwezi Julai 2014 baada ya kuikaimu nafasi ya Umeneja kwa Mechi kadhaa kufuatia kutimuliwa David Moyes katika Msimu wa 2013/14.

Wadadisi wengi wanahisi Giggs ndie anaefaa kuvaa Viatu vya Van Gaal ambae Mkataba wake na Man United unamalizika Juni 2017 lakini Gazeti la England, The Manchester Evening News, limedai Lejendari huyo wa Man United hajatamka kukataa kuondoka Klabuni hapo akipata nafasi murua.

Wachambuzi wengi huko England wamenyooshea kidole Rekosi ya Mwenyekiti wa Swansea, Huw Jenkins, ya kuwapa nafasi Mameneja Vijana baada ya kuwateua Roberto Martinez na Brendan Rodgers huko nyuma na hivyo kumtaka Giggs si kitu cha nje ya falsafa yake.

Wadadisi na Wachambuzi hao pia wamegusia kuwa Giggs kujiunga na Swansea ni kitu chepesi kwa vile Klabu hiyo ni Wales ambayo ni Nyumbani kwao Ryan Giggs.

No comments:

Post a Comment