Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, December 11, 2015

MAN UNITED, LIVERPOOL, SPURS WAPATA WAPINZANI WAO KATIKA RAUNDI YA MTOANO TIMU 32 EUROPA LEAGUE

JANA Mechi za mwisho za Makundi ya UEFA EUROPA LIGI zilikamilika na Timu 24 zilizofuzu kuingia Raundi ya Mtoano ya Timu 32 zilitimia ambazo zitajumuishwa na Timu 8 zilizomaliza Nafasi za 3 kwenye Makundi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI mojawapo ikiwa Manchester United.
Droo ya kupanga Mechi za Raundi ya Mtoano ya Timu 32 ya EUROPA LIGI itafanyika Nyon huko Uswisi Jumatatu Desemba 14 Saa 9 Mchana.

Pamoja na Man United kwenye Droo hiyo zipo pia Liverpool na Tottenham ambao walifuzu kabla ya Mechi za Jana ambapo walikamilisha Ratiba kwa Tottenham, wakiwa Nyumbani, kuichapa Monaco 4-1 na Liverpool kutoka 0-0 na Sion huko Ufaransa.
Bao za Tottenham hapo Jana zilifungwa na Erik Lamela, Bao 3, na Tom Carroll wakati Monaco wakifunga Bao lao kupitia Stephan El Shaarawy.
Jana Timu zilizofuzu kusonga ni Fenerbahçe, Midtjylland, Sion, Marseille, Lokomotiv Moskva, Sporting CP, Fiorentina, Anderlecht, Augsburg na kuungana na Timu nyingine 14 zilizofuzu kabla yake.
Timu hizo zinaungana na Timu 8 zilizotoka UEFA CHAMPIONZ LIGI ambazo ni Man United, Bayer Leverkusen, Olympiacos, Porto, Shakhtar Donetsk, Galatasaray, Sevilla na Valencia.
Kwenye Droo, Timu hizo 32 zimegawanywa kwenye Vyungu Viwili vya Timu 12 kila kimoja huku Chungu Namba 1 kikiwa na Timu zilimaliza Washindi wa Makundi yao pamoja na zile ambazo ziko juu kwenye Listi ya Ubora ya UEFA.

Timu iliyo Chungu Namba 1 itapangwa kucheza na Timu iliyo Chungu Namba 2 isipokuwa Timu za Nchi moja hazitakutanishwa na zile zilizokuwa Kundi moja hazitapangwa kukutana.
Mechi za Raundi ya Mtoano ya Timu 32 zitachezwa Februari 18 na Marudiano ni Februari 25.
DROO-Vyungu-Raundi ya Mtoano ya Timu 32:
Chungu Namba 1: Molde, Liverpool, Krasnodar, Napoli, Rapid Wien, Braga, Lazio, Lokomotiv Moskva, Basel, Tottenham Hotspur, Schalke, Athletic Club, Manchester United*, Bayer Leverkusen*, Olympiacos*, Porto*

Chungu Namba 2: Fenerbahçe, Sion, Borussia Dortmund, Midtjylland, Villarreal, Marseille, St-Étienne, Sporting CP, Fiorentina, Anderlecht, Sparta Praha, Augsburg, Shakhtar Donetsk*, Galatasaray*, Sevilla*, Valencia*
Timu zilizotoka UEFA CHAMPIONS LIGI
EUROPA LIGI

Matokeo Mechi za mwisho za Makundi
Alhamisi Desemba 10
Kundi A

Fenerbahçe 1-1 Celtic
Ajax 1-1 Molde

Kundi B
Bordeaux 2-2 Rubin
Sion 0-0 Liverpool

Kundi C
Qäbälä 0-3 Krasnodar
Dortmund 0-1 PAOK

Kundi D

Midtjylland 1-1 Club Brugge
Napoli 5-2 Legia

Kundi E
Rapid Wien 2-1 Dinamo Minsk
Viktoria Plzeň 3-3 Villarreal

Kundi F
Slovan Liberec 2-4 Marseille
Groningen 0-0 Braga
 

Kundi G
Dnipro 3-0 Rosenborg
St-Étienne 1-1 Lazio 


 Kundi H
Sporting CP 3-1 Beşiktaş
Skënderbeu 0-3 Lokomotiv Moskva


Kundi I
Fiorentina 1-0 Belenenses
Lech Poznań 0-1 Basel

Kundi J
Anderlecht 2-1 Qarabag
Tottenham Hotspur 4-1 Monaco

Kundi K
APOEL 1-3 Sparta Praha
Asteras 0-4 Schalke

Kundi L
Partizan 1-3 Augsburg
Athletic Club 2-2 AZ
KALENDA
Raundi ya Timu 32-Droo: 14 Desemba, Nyon
Raundi ya Timu 32-Mechi ya Kwanza: 18 Februari
Raundi ya Timu 32-Mechi ya Pili: 25 Februari
Raundi ya Timu 16-Droo: 26 Februari, Nyon
Raundi ya Timu 16-Mechi ya Kwanza: 10 Machi
Raundi ya Timu 16-Mechi ya Pili: 17 Machi
Robo Fainali-Droo: 18 Machi, Nyon
Robo Fainali-Mechi ya Kwanza: 7 Aprili
Robo Fainali-Mechi ya Pili: 14 Aprili
Nusu Fainali-Droo: 15 Aprili
Nusu Fainali-Mechi ya Kwanza: 28 Aprili
Nusu Fainali-Mechi ya Pili: 5 Mei
Fainali: 18 Mei, St. Jakob-Park, Basel, Uswisi