Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, October 5, 2015

MESUT OZIL NA ALEXIS SANCHEZ WALIVYOPELEKA KILIO MAN UNITED


Arsenal, wakicheza kwao Emirates, walianza Mechi hii ya Ligi Kuu England vizuri mno na kufanikiwa kuifunga Manchester United Bao 3 ndani ya Dakika 19 za kwanza.
Arsenal walipata Bao la kwanza katika Dakika ya 6 alilofunga Alexis Sanchez na Dakika 1 baadae Mesut Ozil alipiga Bao la pili na kisha Sanchez kufunga Bao la 3 katika Dakika ya 19.
Kwa ujumla Man United kwenye Kipindi cha Kwanza walikuwa goigoi na kuzinduka Kipindi cha Pili lakini walishindwa kufunga Bao lolote.

Matokeo haya yamewafanya Arsenal wakamate Nafasi ya Pili kwenye Ligi wakiwa Pointi sawa na Man United lakini wao wana ubora wa Magoli na wote wako nyuma ya Vinara Man City ambao wana Pointi 16, Pointi 2 mbele ya Arsenal na Man United.
Ligi Kuu England sasa itakaa pembeni kupisha Mechi za Kimataifa na kurejea tena dimbani Oktoba 17.
Shangilia ya aina yake!! Uteja kwishneeyFuraha tupu kwa WengerKila Mtu anashindwa kuaminiFuraha tupu!Sanchez akishangilia moja ya bao lake leoTumemaliza kazi!Mlipuko wa furaha!United Hoi!3-0Van Gaal akijificha uso!Depay akishiliwa Rooney nae yale yale!Meneja Arsene Wenger akitoa maelezo kipindi cha pili
Alexis Sanchez anaipa bao tena la tatu Arsenal na kufanya bao kuwa 3-0 dhidi ya Man United.
Alexis Sánchez anaifungia bao dakika ya 6 na dakika ya 7
Mesut Özil  anatupia bao la pili na kufanya 2-0 dhidi ya Man United kwenye Uwanja wa Emirates.

VIKOSI:
Arsenal: Cech, Bellerin, Mertesacker, Gabriel, Monreal; Coquelin, Cazorla; Ramsey, Ozil, Sanchez; Walcott
Subs: Ospina, Debuchy, Chambers, Gibbs, Oxlade-Chamberlain, Campbell, Giroud

Manchester United: De Gea, Young, Smalling, Blind, Darmian, Carrick, Schweinsteiger, Mata, Rooney, Memphis, Martial
Subs: Romero, Jones, McNair, Schneiderlin, Valencia, Fellaini, Wilson
TIMU ZOTE MBILI WATAOHUKOSA MTANANGE  HUU:
Arsenal: OUT - Koscielny (hamstring), Arteta (thigh), Flamini (hamstring), Wilshere (leg), Rosicky (knee), Welbeck (knee).

Man United: OUT - Rojo (hamstring), Shaw (leg). DOUBTFUL - Carrick (knock), Herrera (knock).

No comments:

Post a Comment