WASANII wa muziki wa kizazi kipya na baadhi ya nyota
wa Bongo Movie watafanya onyesho la bure kesho kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala
kuwahamasisha mashabiki wao kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa
Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25.
Akizungumza jijini jana, Professa J alisema kuwa
sababu kubwa ya kufanya onyesho hilo ni kutoa elimu kwa mashabiki wao kuhusiana
na zoezi la upigaji kura kuchagua viongozi bora wa nchi hii wataodumu kwa miaka
mitano.
“Tumejiandaa kutoa elimu, lengo ni kuwahamasisha
mashabiki wetu kufanya kile wanachokiona kinafaa ili kutimiza malengo yao ya
kikatiba,” alisema Professa J.
Pia alisema wasanii hao wataongozwa na Mbunge wa
Mbeya mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph
Mbilinyi “Sugu” na nyota wengine kama Juma Kassim “Sir Nature”, Joseph Haule
“Professa J” na Kara Jeremiah.
Wengine ni watakaopanda jukwaani siku kuanzia saa
8.00 mchana ni Msaga Sumu, Baba Haji na waigizaji nyota wa Bongo Movie,
Jacqueline Wolper na Auntie Ezekiel.
Professa alisema kuwa wanataka kutoa mwamko kwa
mashabiki wao kushiriki kwa wingi katika zoezi hilo ili kutumia demokrasia yao
kumchagua kiongozi wanayemtaka.
Mbali na Dar es Salaam, onyesho hilo pia litafanyika
katika mikoa mengine mbalimbali.
No comments:
Post a Comment