GOLIKIPA mkongwe nchini Juma Kaseja amesajiliwa na Coastal Union ya Tanga
na ameanza mazoezi.
Akizungumza kwa njia ya simu toka Tanga, Msemaji wa Coastal Union, Oscar
Assenga alikiri ujio wa Kaseja kwenye timu hiyo lakini akasema bado hajasajiliwa
bado wapo kwenye mazungumzo naye.
“Kweli kaseja amekuja Tanga na alionekana kwenye mazoezi yetu juzi lakini
siyo kweli kama amesajiliwa bado yupo kwenye mazungumzo na uongozi endapo
watakubaliana mtataarifiwa”, alisema Assenga.
Habari za ndani zaidi zinasema kuwa, Kaseja tayari ameshamalizana na
Coastal Union na amerejea jijini Dar es Salaam kuchukua vitu vyake tayari kwa
kuanza maisha mapya kwenye klabu ya ‘Wagosi wa Kaya’ msimu ujao.
Hivi karibuni Kaseja alikaririwa akisema klabu za Mbeya City, Mwadui FC
na Ndanda zilikuwa zikiwania saini yake baada ya TFF kumruhusu kujiunga na timu
yoyote baada ya kupitia maombi yaliyoletwa kwao na Chama cha wacheza Soka
Tanzania (SPUTANZA) kikiomba mchezaji huyo kuwa huru na kujiunga na klabu
yoyote wakati akisubiri hatma ya kesi yake na Yanga kwani hawajamwondoa kwenye
mgogoro wa kikazi na klabu yake.
Ikiwa Coastal Union watafanikiwa kuinasa saini ya Golikipa huyo wa zamani
wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Simba na Yanga watakuwa wamelamba
dume kutokana kuwa kwenye ubora kwani anafanya mazoezi kwenye mafunzo
yanayoendeshwa na Peter Manyika kwenye Uwanja wa Karume kila siku asubuhi.
No comments:
Post a Comment