MSANII wa muziki wa kufoka foka toka Kikosi cha Mizinga, Karama
Masoud, amechukua fomu za kugombea udiwani
kwenye kata ya Kinondoni jijini Dar es Salaam juzi.
Karama maarufu kama Kalapina, anagombea udiwani kupitia chama cha ACT
Wazalendo.
Akizungumza baada ya kuchukua fomu hizo, Kalapina alisema kuwa ameamua
kugombea udiwani ili kuleta mabadiliko kwa vitendo kwani anaamini anaweza
kuongoza kata ya Kinondoni.
“Najiamini kama kijana kuwa na naweza hivyo nimejiandaa kuleta mabadiliko
nikishirikiana na wananchi wa Kinondoni”, alisema Kalapina huku akishangiliwa
na waendasha bodaboda ambao walimsindikiza.
Pia Kalapina alisindikizwa na katibu kata
tawi la Kinondoni wa ACT, Johnson Kapi.
Kalapina ambaye pia ni kiongozi wa kundi la Kikosi Cha Mizinga, Mei
alitangaza kugombea
ubunge kupitia Chama cha Wananchi, CUF jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment