CHAMA cha Soka Dar es Salaam (DRFA) kimewaomba wapiga kura wote kujitokeza kwenye
uchaguzi wa kuwapata viongozi watakaokiongoza chama cha soka Temeke (TEFA) ili
kuleta maendeleo ya mpira wa miguu mkoa wa Dar es salaam.
Wito huo umetolewa na Msemaji wa
Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam, (DRFA) na kusisitiza amani na utulivu
itawale katika zoezi hilo muhimu la upigaji kura.
“Shirikisho la mpira wa miguu nchini
TFF limekiruhusu chama cha soka mkoa wa Dar es salaam (DRFA) kuendelea na mchakato wa uchaguzi wa viongozi
wa chama cha soka wilaya ya Temeke (TEFA) kama ulivyopangwa na kamati ya
uchaguzi ya chama hicho hivyo tunawasihi wanachama na wagombea kudumisha
amani”, alisema Katanga.
Baada ya ruhusa hiyo Uongozi wa DRFA
umemuandikia barua katibu wa TEFA Kasim Mustapha ili aijulishe kamati ya
uchaguzi ya chama hicho kuendelea na mchakato huo kama kawaida.
Awali TFF iliiandikia barua DRFA
kushauri kusimamishwa kwa uchaguzi huo, kutokana na kile kinachoonekana kuwepo
na malalamiko kuhusu mchakato wake lakini baada ya mashauriano kati ya pande
hizo mbili, sasa ni ruksa kwa uchaguzi huo kufanyika kesho (leo) jumapili kama ulivyopangwa.
No comments:
Post a Comment