UONGOZI wa Klabu ya Rangers, ambayo inashiriki ligi daraja la kwanza Tanzania bara, umedhamiria
kurekebisha makosa ya msimu uliopita’
Akizunmgumza jijini, kocha mkuu, Herry Mzozo alisema msimu uliopita
walifanya vizuri mzunguko wa kwanza wakiongoza kundi lao lakini mzunguko wa
pili wakijikuta wanaporomoka na kumaliza wakishika nafasi ya tatu na
kuzipisha klabu kongwe za Africans
Sports ya Tanga na Majimaji ya Songea kupanda ligi kuu
Maneno ya Mzozo yalitiwa nakshi na na mchezaji wa zamani wa Kimataifa wa Tanzania na klabu za Simba na Yanga, Ally Yusuph ‘ Tigana’, ambaye ni kocha msaidizi, Meneja wa timu Kassim Siwa timu yao itapanda ligi kuu licha ya kukwama katika hatua za mwisho msimu uliopita.
Mzozo alisema timu ina wachezaji nyota katika mpira ambao ni Credo Maipopo, Haruna Moshi ‘ Boban’, Amir Maftah, Yusuph Mgwao, Stephano Mwasyika na rundo la wachezaji vijana.
Pia alisema amejifunza mengi kwenye ligi likiwa ni kuwa mpira wa Tanzania siyo uwanjani tu kwani klabu zenye pesa utoa rushwa kwa waamuzi na viongozi ndiyo zinapanda huku wanaojua wanaachwa, soka linaangamia, siasa imetawala
No comments:
Post a Comment