TIMU
ya ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars)
iliyooweka kambi kisiwani Zanzibar, kujiandaa na fainali za Michezo ya Afrika
(All Africa Games) imeendelea kujifua kutwa mara mbili katika viwanja wa Aman
na Fuoni kabla ya safari ya kuelekea nchini Congo – Brazzavile mwezi ujao.
Akizungumza
jijini, Ofisa habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, Baraka Kizuguto alisema
Twiga Stars ambayo chini ya Kocha Mkuu Rogasian Kaijage inaendelea vema na
maandalizi ya mchezo wa kirafiki na timu ya Taifa ya Kenya (Harambee Starlets)
Agosti 23 katika uwanja wa Amani kisiwani Zanzibari.
“Kaijage
amesema anashukuru vijana wake wanafanya mazoezi kwa morali ya hali ya juu na
wanaonekana kuyashika vizuri mafunzo yake na kumpa imani kuwa sasa kikosi chake
kimeiva na anachosubiri ni mchezo wa kirafiki dhidi ya Kenya ili kuweza kuona
uwezo wa kikosi chake kabla ya safari ya kuelekea nchini Congo-Brazzavile”,
alisema Kizuguto
Naye
Blassy Kiondo ambaye ndie mkuu wa msafara timu ipo katika hali nzuri, wachezaji
wanafanya mazoezi kwa morali ya hali ya juu, hakuna majeruhi kikubwa
wanachosubiri kwa sasa ni huo mchezo wa kirafiki dhidi ya Kenya.
Wakati
huo huo, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi
ametuma salamu za pongezi kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini
Burundi (FBF) Reverien Ndikuriyo kwa kuchaguliwa kuwa spika wa bunge la Seneta
nchini humo.
Katika
salam hizo za pongezi kwa Rais wa FBF na nakala zake kwenda CECAFA, CAF na
FIFA, Malinzi ameelezea imani yake kwa Seneta Ndikuriyo na amemtakia kila la
kheri na mafanikio katika nafasi hiyo mpya aliyochaguliwa.
No comments:
Post a Comment