UONGOZI wa
klabu ya Ashanti United, umesema umejipanga kuhakikisha timu yao inarejea
kwenye ligi Kuu Tanzania Bara, msimu huu.
Akizungumza
jijini Msemaji wa Ashanti, Marijani Rajab alisema wamefanya usajili mzuri ambao
utaleta upinzani mkali uwanjani japo kuna nafasi kandaa za kuziba.
“Timu
imeshaanza mazoezi chini ya kocha Maalimu Salehe na tumefanya usajili wa
uhakika kutokana na mahitaji ya kocha lakini kuna nafasi mbili ambazo zina
mapungufu ambazo tunatarajia kuzifanyia kazi mapema”, alisema Marijani.
Pia
aliwataka wanachama na wapenzi wa Ashanti kufika kwenye mazoezi yanayofanyika
kwenye Uwanja wa Msimbazi Rovers, Ilala kila siku jioni kujiona vijana
waliosajiliwa.
Ligi daraja
la kwanza (FDL) inatarajiwa kuanza Septemba 17 huku ligi daraja la pili ikitarajiwa
kuanza Oktoba 16 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment