Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, August 12, 2015

DAVID DE GEA KUBAKI OLD TRAFFORD, REAL WAKIMTAKA WATOE PAUNI 32.6M

KIPA kutoka Spain David De Gea anatarajiwa kubakia Manchester United na si kuhamia Real Madrid kama wengi wanavyotarajia.
De Gea, mwenye Miaka 24, hakuwemo kwenye Kikosi cha Man United ambacho Jumamosi kiliifunga Tottenham 1-0 kwenye Mechi ya kwanza ya Ligi Kuu England Msimu huu baada ya Meneja Louis van Gaal kuamua kuwa Kipa huyo hayupo fiti kisaikolojia kutokana na kuzongwa na fikra za kuhamia Real Madrid.

Msimamo wa Man United kuhusu Kipa huyo kuhamia Real ni kuwa anaweza kwenda ikiwa tu Klabu hiyo ya Spain italipa Dau la Rekodi ya Dunia kwa Kipa ama pale Beki wa Real Sergio Ramos, mwenye Miaka 29, akija Old Trafford.

Rekodi ya Dunia kwa kununuliwa Kipa ni Pauni Milioni 32.6 ambayo Juventus walilipa kumnunua Gianluigi Buffon Mwaka 2001 kutoka Parma. KIPA kutoka Spain David De Gea anatarajiwa kubakia Manchester United na si kuhamia Real Madrid kama wengi wanavyotarajia.
De Gea, mwenye Miaka 24, hakuwemo kwenye Kikosi cha Man United ambacho Jumamosi kiliifunga Tottenham 1-0 kwenye Mechi ya kwanza ya Ligi Kuu England Msimu huu baada ya Meneja Louis van Gaal kuamua kuwa Kipa huyo hayupo fiti kisaikolojia kutokana na kuzongwa na fikra za kuhamia Real Madrid.
www.bukobasports.com

Lakini hivi sasa Maafisa wa Man United wanaamini hayo yote mawili hayawezi kutokea kabla ya Septemba Mosi wakati Dirisha la Uhamisho likifungwa na hivyo De Gea atabakia Old Trafford.
Kuelekea Msimu huu mpya, De Gea aliwahi kuidakia Man United Mechi mbili za Kirafiki huko USA dhidi ya Barcelona na Paris St-Germain.


Jumamosi, kwenye Mechi na Tottenham, Kipa mpya ambae huidakia Timu ya Taifa ya Argentina, Sergio Romero, mwenye Miaka 28, ndie alikaa Golini ikiwa ni Mechi yake ya kwanza kwa Man United.
Baada ya Mechi hiyo ya Ligi Kuu England, Van Gaal alisema upo uwezekano wa De Gea kuidakia tena Man United lakini atafanya tathmini baada ya Dirisha la Uhamisho kufungwa.
Van Gaal alisema: “Yeye ndie Mchezaji wetu Bora kwa Misimu miwili iliyopita hivyo hatuwezi kumwacha aondoke kirahisi. Tunataka kumuuza kiwango kile kile tunachouziwa Wachezaji. Lakini tunataka abaki.”
Sakata la Makipa la Man United pia linamhusu Anders Lindegaard ambae nae ameruhusiwa kuondoka huku Kipa mwingine kutoka Spain, Victor Valdes, akiwekwa kwenye Listi ya kuuzwa baada ya Van Gaal kudai aligoma kuichezea Timu ya Rizevu.
Kipa wa Tatu wa Man United ni yule anaechezea Timu ya Taifa ya England ya U-21, Sam Johnstone, ambae alikuwa aende kwa Mkopo huko Preston lakini kutokana na hali ya kutojulikana hatima za Makipa wengine Mkopo wake umesimamishwa.

No comments:

Post a Comment