Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, August 5, 2015

MAANDALIZI YA TWIGA STARS INAYOKWEDA KUPAMBANA NA NIGERIA, CONGO NA IVORY COAST KAMA TUNATANIA

Kocha wa mkuu wa Twiga Stars Rogasian Kaijage akizungumza na waandishi wa habri leo kwenye ofisi za TFF

Kocha wa mkuu wa Twiga Stars Rogasian Kaijage akizungumza na waandishi wa habri leo kwenye ofisi za TFF
Timu ya Taifa ya wanawake ‘Twiga Stars’ ipo kambini kwenye hosteli za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ikifanya maandalizi ya mwisho kabla ya kuelekea nchini Congo Brazzaville kushiriki michuano ya All Africa Games ambapo timu hiyo ilifuzu kwa kuiondosha Zambia ‘Shepolopolo’ na kukata tiketi ya kushiriki michuano hiyo.
Kocha mkuu wa timu hiyo Rogasian Kaijage alikuwa ameomba aandaliwe mazingira kwa ajili ya kuiandaa timu hiyo kwa muda mrefu kwa kuwaweka wachezaji kambini kwa vipindi tofauti huku wakipata michezo kadhaa ya kirafiki ya kimataifa lakini mambo yamekuwa magumu kutokana na hali ya uchumi kutoruhusu hayo yote kufanyika.
Timu hiyo iliingia kambini Julai 15 mwaka huu ikiwa na mchanganyiko na timu ya vijana ambao walikuwa wanajiandaa kwa mechi ya marudiano dhidi ya Zambia na baada ya wachezaji wa timu ya vijana kwenda Zambia, wachezaji waliobaki waliendelea na mazoezi chini ya mwalimu aliyebaki. Baadae, wachezaji wa timu hiyo waliruhusiwa kwenda kujiandikisha kwa ajili ya kupiga kura na baadae kurudi tena kambini baada ya siku tatu.
Kundi A ambapo Twiga Stars imepangwa kwenye michuano ya All Africa Games
Kundi A ambapo Twiga Stars imepangwa kwenye michuano ya All Africa Games
Awali mwalimu aliomba timu hiyo ipelekwe Zanzibar kwa ajili ya kuweka kambi huko lakini pia hilo limeshindikana kutokana na ukosefu wa fedha ambapo timu hiyo ilitegemewa kuondoka kuelekea visiwani Zanzibar humo.
Lakini Kaijage amesema yeye anaendelea na ratiba yake ya mazoezi kama alivyoipanga licha ya kushindwa kwenda Zanzibar kuweka kambi huko japo amesema jambo hilo linaweza linaweza kuwaathiri kisaikolojia baadhi ya wachezaji kwasababu walikuwa wanajua wataenda kukaa mahali fulani na walikuwa wamefurahia jambo hilo.
Amesema kambi ya Karume sio nzuri sana kutokana na eneo kuwa na mwingiliano mkubwa na watu wengine pamoja na mashabiki ambao huenda kuangalia mazoezi ya timu nyingine zinazoutumia uwanja huo kwa ajili ya mazoezi.
Hii ndio ratiba ya mechi za kundi A
Hii ni ratiba ya mechi za kundi A
Twiga Stars haina mdhamini kama ilivyo Taifa Stars, Twiga inategemea kila kitu kutoka TFF. Ikumbukwe timu hii inaenda kushiriki michuano mikubwa ya Afrika na itakutana na timu zenye majina makubwa barani Afrika ambazo zimeandaliwa kwa ajili ya kupambana kutwaa ubingwa.
Kwa namna inavyoandaliwa timu hii haioneshi kama tunataka kwenda kuleta changamoto kwenye mashindano hayo mbali na kushiriki kisha kurejea nyumbani. Kuna haja kubwa ya kuwekeza kwenye soka la wanawake kwasababu wameonesha wanaweza na ndio maana wamefuzu kushiriki kwenye fainali hizo.
Timu itakapofanya vibaya lawama zote zitaelekezwa kwa kocha na yeye ndie atakaeubeba mzigo wa lawama zote endapo timu hiyo itafanya vibaya, lakini kuna swali la kujiuliza kabla ya kumlaumu kocha wa Twiga kama timu haitafanya vizuri, tumewekeza kwa kiasi gani kwa Twiga Stars mpaka tunataka matokeo mazuri?
Baada ya kupata jibu la swali hilo  hapo ndipo tuanze kumnyooshea kidole kocha kwa matokeo mabovu atakayoyapata akiwa huko.
Rekodi za timu za kundi A
Rekodi za timu za kundi A
Wachezaji wengi wa Twiga hawana timu na Tanzania hakuna ligi ya wanawake hivyo wachezaji hao walitakiwa kukaa kambini kwa muda mrefu na kupata mechi nyingi za kirafiki za kimataifa na timu zenye uwezo sawa au unaokaribiana na timu ambazo Twiga itaenda kupambana nazo kwenye michuano ya All Africa Games.
Tanzania ipo kundi A pamoja na Conco Brazzaville ambao ndio wenyeji wa michuano hiyo, Nigeria na Ivory Coast. Congo, Tanzania na Ivory Coast ni timu ambazo zinashiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza wakati Nigeria inashiriki michuano hiyo kwa mara ya tatu na imewahi kutwaa medali ya dhahabu mara mbili mwaka 2003 na 2007.

No comments:

Post a Comment