Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, August 5, 2015

HII NDIO DERBY YA SHINYANGA, JUMAMOSI KAMBARAGE SIYO YA KUKOSA



TIMU za Stand United na Mwadui FC za Shinyanga zinatarajiwa kufungua dimba la mashindano maalum yanayozikutanisha timu za ligi kuu zilizopo kanda ya ziwa Victoria siku ya jumamosi kwenye uwanja wa Kambarage Shinyanga.
Mashindano hayo yameandaliwa na Chama cha Soka Shinyanga (SHIREFA), kwa kushirikiana na kampuni ya Cleverland Res ya Mwanza na yatazikutanisha timu zote zilizopo ligi kuu za ukanda huo
Akizungumza jijini Mratibu wa mashindano hayo, Kabole Kahungwa alisema michuano hiyo itakuwa ikichezwa kila siku kuanzia Agosti 8-12 kwa mtindo wa ligi ili kuzipa maandalizi timu za Kanda ya Ziwa kabla ya Ligi Kuu.
“Kama unavyoona timu za Kanda ya Ziwa zimefanya usajili mzuri kuelekea Ligi Kuu, kwa hivyo na sisi tumeona tuziandalie mashindano baina yao ili kujiweka fiti, kabla ya ligi kuu kuanza”, amesema Kahungwa.
Pia alizitaja timu hizo kuwa ni Stand United, Mwadui FC zote za Shinyanga, Toto African ya Mwanza na Kagera Sugar ya Kagera.
Ligi Kuu inatarajiwa kuanza  Septemba 22,  huku kanda ya Ziwa msimu huu ikiwa na timu nne, baada ya Toto African na Mwadui FC kupanda msimu huu na kuungana na Kagera Sugar na Stand United.
Ratiba ya mashindano hayo ni kama ifuatavyo, Agosti 8 ni Stand United Vs Mwadui FC, Agosti 9 ni Toto African Vs Kagera Sugar, Agosti 10 ni Mwadui FC Vs Toto Africans, Agosti 11 ni Kagera Sugar Vs Stand United, Agosti 12 ni Stand United Vs Toto African na Agosti 13 ni Mwadui FC Vs Kagera Sugar

No comments:

Post a Comment