Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, August 5, 2015

KASEJA HUYOOOOOO MWADUI FC



ALIYEWAHI kuwa golikipa wa vilabu vya Simba na Yanga, Juma Kaseja na mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Jerryson Tegete huenda wakajiunga na klabu ya Mwadui FC kwa msimu huu.
Hayo yamesemwa na Kocha Mkuu wa klabu hiyo Jamhuri Kihwelo na kusema kama mambo yataenda kama yalivyopangwa atawasajili ili waweze kuonyesha uwezo wao mkubwa.
 “Mimi nimeshasajili wachezaji 26 wanatosha, lakini wachezaji pekee ambao kama mipango yangu itaenda sawasawa basi kuna mpango wa kuwaongeza ni Juma Kaseja na Jerry Tegete kwasababu ni wachezaji ambao nimezungumza nao na wameniambia wanataka kucheza na hawakuweka mbele kipato, na wamenivutia, tunataka tuwatumie kucheza ili tupate mafanikio kwenye ligi”.
Julio pia aliweka wazi kuwa kuna wachezaji ambao uwezo wao ni mdogo hivyo inabidi wawatoe kwenye dirisha dogo la usajili, lakini ukiwa na wachezaji wazuri wenye kuonesha uwezo na wanataka kucheza kuisaidia timu yao sioni kwanini asiwachukue kwa vile bado hajamaliza usajili wote.
Pia alisema usajili wa wachezaji wa kigeni unaofanywa na baadhi ya klabu hapa nchini haumtishi kwani yeye ni kocha mkubwa na anatambua uwezo wa wachezaji wengi na hata pale anapowaita wachezaji anaangalia uwezo wa mchezaji na si umri.
 “Mimi sitishiki na usajili wa Azam, Simba na Yanga, wao wamevutika na wachezaji wa nje kwasababu zao binafsi na kwa sababu wana fedha pia Yanga wanatarajia wakiwa na wachezaji wa kigeni watafanikiwa kwasababu wanacheza mashindano ya Afrikahivyo wanataka kuingia kwenye nane bora ‘Super eight’ lakini sidhani kama hilo litafanikiwa”, alisema Julio
Pamoja na maneno mengi Julio alionesha kuukubali usajili  wa Azam na kusema juzi wamefanya vizurui kuchukua ubingwa na kukiri timu hiyo sio mbaya lakini akasema Simba wao wanataka kuchukua ubingwa ambao wameupoteza kwa takribani miaka mitatu

No comments:

Post a Comment