Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, July 24, 2015

YANGA YATINGA ROBO FAINALI BAADA YA KUIFUNGA KMKM LEO




Yanga imefanikiwa kuingia robo fainali ya michuano ya Kagame ikitokea Kundi A baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya KMKM.
Katika mechi hiyo ambayo ilikuwa ya kasi kubwa, Yanga ilipata ushindi huo kwa bao lililofungwa na Malimi Busungu kipindi cha pili
Baadae kidogo beki wa KMKM alijichanganya wakati wakigombea mpira uliopigwa na Amissi Tambwe na kumpita kipa Nassor Abdullah na kuandika bao la pili.
KMKM wakitoa upinzani mkali ingawa katika dakika 30 za mwisho, walionekana kulishinda kuhimili mikikimikiki ya Yanga.
Yanga imefikisha pointi sita baada ya kucheza mechi tatu, ikiwa imepoteza mchezo mmoja dhidi ya Gor Mahia.
Itamaliza mechi ya mwisho dhidi ya Al Khartoum yenye pointi saba, Jumapili. Iwapo itashinda itakuwa imefikisha pointi 9 na kuwa katika nafasi ya pili au ya kwanza ingawa itasubiri pia matokeo ya Gor Mahia na Telecom.
Katika mechi ya kwanza leo, Gor Mahia ilitoka sare ya mabao 1-1 dhidi ya Al Kharthoum.

No comments:

Post a Comment