Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, July 30, 2015

MTOTO HUYU ANATAFUTWA NA HIMID MAO WA AZAM FC


Himid MaoBaada ya timu yake kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya CECAFA  Kagame Cup, kiungo mahiri wa Azam FC Himid Mao ameposti picha ya mtoto mdogo wa kike ambae alipigwa picha akiwa uwanjani akishuhudia mchezo wa robo fainali kati ya Yanga na Azam ambapo Azam walishinda kwa mikwaju mitano ya penati dhidi ya mitatu ya Yanga.
Picha hiyo iliambatana maneno yafuatayo: “My favorite picture for today (picha yangu bora kwa leo) mwenye mtoto huyu  huyu anitafute nina zawadi yake”, mwisho wa kumnukuu Mao.Himid Mao new
Wachezaji wa Azam wameonekana kufurahia kuitupa nje timu ya Yanga ambayo imekuwa ikiwapa tabu pindi wanapokutana na historia inaonesha Azam na Yanga zinapokutana basi mara nyingi Yanga huibuka na ushindi. 
Kwenye mchezo huo, Mao alicheza kwa dakika zote 90 na alikuwa miongoni mwa wachezaji waliopiga penati ambapo yeye alipiga penati ya tatu na kufunga.
Mao anamtafuta mtoto huyo ili ampe zawadi japo hajaitaja ni zawadi gani, kwa mtu yeyote anayemfahamu mtoto huyo, wazazi wake au mtu wa karibu na mtoto huyo basi anaweza kutoa taarifa kwa watu hao ili wawasiliane na Mao ili waweze kupatiwa zawadi hiyo.

No comments:

Post a Comment