Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, March 14, 2015

MAJONZI!!!!!!!! MARSHI HATUNAYE TENA



 
ALIYEKUWA kocha Msaidizi wa timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars, Sylvester Marsh ameaga dunia jana alfajiri katika hospitali ya Muhimbili alikokuwa amelazwa.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu toka Morogoro kwenye Mkutano Mkuu wa TFF, Katibu wa chama cha Makocha, Michael Bundala alisema kuwa chama kimepokea taarifa za msiba huo kwa masikitiko kwani ni moja ya makocha ambao bado wanahitajika nchini ila kazi ya Mungu haina makosa.

“Tumepata hizo taarifa za kifo cha mwenzetu, kiukweli zimetuhuzunisha kwani bado mchango wake unahitajika na kati ya makocha ambao wanahitajika kutokana na kuipenda kazi yake na kuzingatia maadili ila  hatuna jinsi”, alisema Bundala kwa sauti yenye kusikitika.

Marsh ambaye nyumbani kwake ni Mwanza taarifa zinasema alikuja Muhimbili kuhudhuria kliniki ya kawaida ya ugonjwa wa  saratani ya koo ambayo iligundulika alipolazwa awali Muhimbili na kufanyiwa upasuaji na baadae kuhurusiwa kurudi nyumbani lakini ghafla hali yake ikabadilika ndio umauti ukamfika.

Marsh alianza kuwa Kocha Msaidizi wa timu za vijana Tanzania mwaka 2003 chini ya Abdallah Athumani Seif  ‘Kibadeni’  na mwaka 2006 apandishwa timu ya wakubwa, alianza kumsaidia, Marcio Maximo na baadaye, Jan Poulsen na Kim Poulsen ambao wote ni raia wa Dernmark

Baada ya Jamal Malinzi kubadilisha benchi la ufundi la Taifa Stars,  Marsh alirudi Mwanza kufanya kazi kwenye kituo chake kinachojulikana  kama Marsh Academy kabla ya kuanza kuugua lakini aliendelea kufundisha wakati akipata ahueni

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Jamal Malinzi, alibadilisha benchi la ufundi Oktoba mwaka jana, na Marsh aliondoka pamoja na Kim Poulsen ambaye alikuwa kocha Mkuu ambapo  Sasa nafasi yake ilichukuliwa na Mart Nooij raia wa Uholanzi na msaidizi wake ni Salum Mayanga.

Ukiacha timu za Taifa, Marsh amewahi kufundisha klabu za Toto African ya Mwanza, 82 Rangers ambayo ilikuja kuitwa Kahama United, Geita Gold Mines, Kagera Sugar ya Kagera na Azam FC ya Dar es Salaam na akiwa na Kagera Sugar, mwaka 2004 aliweza kutwaa kombe la Tusker.

Pia akiwa Msaidizi wa Kibadeni katika U17, maarufu kama Serengeti Boys, Mwaka 2004, waliiwezesha timu hiyo kukata tiketi ya kucheza Fainali za Afrika nchini Gambia, baada ya kuzitoa Rwanda, Zambia na Zimbabwe hata hivyo Tanzania ilikuja kuenguliwa kwa kashfa ya kumtumia Nurdin Bakari aliyekuwa amezidi umri.

Pia alikuwa Mkufunzi wa soka, Marsh atakumbukwa kwa msimamo wake na uzalendo alipokuwa kocha sehemu zote alizopita. Bwana ametoa, bwana ametwaa. Jina lake libarikiwe. 

No comments:

Post a Comment