KOCHA wa
zamani wa Simba SC, Zdravko Logarusic ameteuliwa kuifundisha, AFC Leopards ya Kenya
na tayari ameshatua kuanza kibarua hicho.
Logarusic ambaye
ni raia wa Crotia ametua Kenya, juzi jioni saa 12:30 kwa madaha kwenye Uwanja wa
Kimataifa wa Jomo Kenyatta huku akiwa mawani mazito ya jua.
Akizungumza
na gazeti hili kwa njia ya mtandao wa kijamii wa facebook, Zdravko Logarusic
alisema amekwenda Kenya baada ya mapumziko baada ya Simba ya Dar es Salaam
kumtupia virago
“Nafurahi
kurejea Kenya kwani naamini kazi niliyoifanya nikiwa na Gor-Mahia wengi
walivutiwa nayo naamini hata Tanzania kipindi nilichokuwa na Simba mashabiki
walivutiwa na kiwango changu cha ufundishaji ila siasa za mpira ndo zinafanya
kocha waondoke kwenye vilabu na kujikuta wanakurudi tena”, alisema Loga
Logarusic
kocha mwenye kujiamini alipokelewa na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Allan Kasavuli
na Katibu msaidizi, Asava Kadima na ameshajiunga na timu kambini Mumias,
magharibi mwa Kenya ambapo ilikuwa na kocha msaidizi, Yusuf Chippo
Logarusic anakuwa
na kibarua cha kwanza leo baada ya AFC Leopards itakapokuwa ikicheza dhidi ya Chemelil Sugar nyumbani kwao, ambapo pazia la Ligi Kuu ya
Kenya litakuwa likifunguliwa rasmi licha ya mgogoro unaoendelea na Shirikisho
la Soka Kenya, FKF, kuhusu idadi ya timu zitakazoshiriki ligi hiyo.
‘Loga’, ambaye amewahi kuzifundisha klabu za Ashanti Gold na King Faisal FC za Ghana pamoja Gor Mahia ambao wapinzani wa Leopards ya Kenya na Simba ya Dar es Salaam amefurahi kurejea Kenya ujio ambao mashabiki wameupokea kwa furaha
‘Loga’, ambaye amewahi kuzifundisha klabu za Ashanti Gold na King Faisal FC za Ghana pamoja Gor Mahia ambao wapinzani wa Leopards ya Kenya na Simba ya Dar es Salaam amefurahi kurejea Kenya ujio ambao mashabiki wameupokea kwa furaha
No comments:
Post a Comment