Timu ya Red Arrows |
Timu ya Kiluvya FC |
Benchi la Red Arrows |
Waamuzi na manahodha wa mchezo |
Benchi la Kiluvya Fc |
TIMU ya
Kiluvya FC, ya Pwani imejikuja ikipokea kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Red
Arrows ya Zambia kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliochezwa Uwanja wa
Karume jijini Dar es Salaam juzi.
Kiluvya FC
ambao wanaongoza Ligi Daraja la pili bila kufungwa walijikuta wakipokea kipigo
hicho toka kwa wageni hao ambao wanacheza ligi Kuu ya Zambia ambao wapo nchini
kujiandaa na Ligi yao.
Jahazi la
Kiluvya lilianza kuzama dakika ya 27 baada ya mshambuliaji Testus Mbwewe
kufunga bao kwa ustadi kwa kuwazidi mbio mabeki wa Kiluvya hali iliyowafanya
kuzinduka na kuanza kushambulia lakini walijikuta wakienda mapumziko bila
kubadili matokeo hayo.
Kipindi cha
pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko ambapo Red Arrows walitoa
wachezaji saba na kuingiza wengine saba hali iliyozindisha umakini kwani dakika
ya 53 mshambuliaji Brenson Chama aliongeza bao la pili baada ya kipa wa Kiluvya
FC kutema mpira na yeye kuutia wavuni bila ajizi.
Baada ya bao hilo Kiluvya walijitahidi
kuanzisha mashambulizi lakini ukuta wa Red Arrows uliojengwa na wachezaji wenye
miili mikubwa na warefu wa kimo ulikuwa kikwazo kwao kwani ulikuwa haupitiki.
Red Arrows
walionekana kumiliki mpira huku pasi zao zikiwa za haraka haraka walifanya shambulizi
dakika ya 75 na kufanikiwa kupata bao la tatu lililofungwa na mshambuliaji wa
Daniel Sibanda baada ya kuwazidi mbio mabeki wa Kiluvya wakidhani ameotea.
Baada ya
mchezo huo kocha wa Red Arrows Mathew Phiri, alisema kikubwa anachojengwa kwa
wachezaji wake ni mchezo wa kushirikiana na pasi za haraka hivyo mechi za
kirafiki zitasaidia kupima uchezaji wa kila mchezaji.
“Tumeweka
kambi Tanzania ili wachezaji waone mazingira mapya ambayo yatakuwa yakiwafanya
akili kutulia ili ninachofundisha wakielewe zaidi kuliko wangekuwa kwenye
mazingira yaleyale ya siku zote”, alisema Phiri
Naye kocha
wa Kiluvya FC, Yahaya Issa alisema matokeo ya kufungwa wanayachukulia kama
changamoto kwao pia alisema wachezaji wake waliogopa mechi na walikuwa
wakichelewa kutoa pasi jambo lilisababisha kupoteza pasi kwani wapinzani
walikuwa wepesi kujipanga kuzuia wakipoteza mpira.
No comments:
Post a Comment