WACHEZAJI wa zamani wa Simba wameandaa mchezo wa kirafiki
wenye lengo la kumchangia mchezaji mwenzao Christopher Alex anayesumbuliwa na
maradhi ya kifua kikuu.
Mchezo huo utachezwa kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es
Salaam Januari 14, mwaka huu, dhidi ya veteran wa Yanga na kiingilio kitakuwa
2000.
Akizungumza jijini mchezaji wa zamani wa Simba, Boniface
Pawasa amewaomba mashabiki wa soka kujitokeza kwa wingi ili kumchangingia
mchezaji huyo ambayo ni miongoni wachezaji walioifunga Zamalek 2003.
“Ninawaomba mashabiki waje kwa wingi ili kumchangia mchezaji
mwenzetu apate pesa ya matibabu na kujikimu kuliko kujitokeza kumchangia wakati
akiwa amekufa kwani kwa kufanya hivyo tutakuwa tumeonyesha kuwa michezo kweli
ni undugu”, alisema Pawasa.
Naye Juma Kaseja ambaye akiwa miongoni mwa wachezaji
waliokuwepo kwenye kikosi hicho maarufu kama Simba ya Zamalek amewaomba wote
waungane kumchangia mwenzao kwani, maradhi au matatizo yameumbwa kwa ajili ya
wanadamu hivyo kusitiriana ni muhimu.
Christopher Alex anasumbuliwa na maradhi ya kifua kikuu
ambayo yanafanya afya yake kudhoofika, hivi sasa yupo nyumbani kwao Dodoma.
No comments:
Post a Comment