KOCHA wa Stand United ya Shinyanga, ‘Chama la Wana’ Mganda,
Mathia Lule, amejigamba kuifunga JKT Ruvu kwenye mchezo utakaochezwa Jumamosi
kwenye Dimba la Chamazi jijini Dar es Salaam.
Lule ambaye amewahi kuzinoa timu za KCCA, Express na timu ya
Taifa ya Vijana ya Uganda U-17 amesema kikosi chake kipo vizuri na kina morali
ya hali ya juu hivyo ushindi ni haki yao
“Timu ipo vizuri hata wewe mwandishi waweza ona vile
wanavyofanya mazoezi, ushindi ni wetu”, alisema kocha huyo kwa Kiswahili chanye
lafudhi ya Kiganda
Pia alisema usajili waliofanya dirisha dogo umefanya timu
ibadilike kiuchezaji na ufundi na kuwataka wapinzani wakae mkao wa kupata
kichapo kila watakapo kutana nao.
Naye kiungo mshambuliaji Haroun Chanongo aliyesajiliwa
dirisha dogo akitokea Simba ameonekana kufanya vizuri kwenye mazoezi
yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam jana.
Chanongo ambaye alikuwa akichezesha kwa tahadhari asiumie
alifunga mabao mawili kati ya matatu kwenye mazoezi hayo hali iliyofanya
wachezaji na mashabiki waliokuwepo kumpongeza.
Lule ambaye anasaidiwa na Athuman Bilal na Emanuel Massawe
amesema anafurahia kazi yake kwani anapata ushirikiano toka kwa uongozi,
makocha wenzake na wachezaji pia.
No comments:
Post a Comment