Kocha wa Polisi Mara, Henry Mkanwa akionyesha vitu vyake kwa wachezaji walipokuwa wanafanya mazoezi Uwanja wa Karume jijin iDar es Salaam |
Kikosi cha Polisi Mara |
KOCHA wa
Polisi Mara, Henry Mkanwa amejigamba kuipandisha timu yake kucheza Ligi Kuu
Tanzania Bara kwa msimu ujao.
Mkanwa
aliyasema hayo jijini Dar es Salaam ambapo timu yake imeweka kambi kwa ajili ya
kujiandaa na mchezo wa Januari 7, mjini Morogoro.
“Nimejipanga
kuhakikisha timu yangu inapanda kucheza ligi Kuu kwa msimu ujao kwani timu yetu
ni nzuri na wachezaji wana morali”, alisema Mkanwa ambaye alishawahi kuchezea
Reli ya Morogoro
Pia alisema
Polisi kwa sasa ina pointi 18 ipo kwenye nafasi ya tano ikiwa imebakiza michezo
saba, mitano ya nyumbani na miwili ya
ugenini atahakikisha wanashinda michezo
yote ili aweze kushika nafasi kati ya nafasi mbili za juu zitakazo mwezesha
kucheza Ligi Kuu au hata kupata best looser ambaye ataungana na washindi wawili
wa juu kutoka katika kundi ilikufikisha timu tano za kuingia Ligi Kuu.
“Kila kundi
zinapita timu mbili na timu moja inaingia kama best looser hivyo nitahakikisha
napata nafasi ya kucheza Ligi Kuu kwani timu yangu ni bora na wachezaji wana
morali”, alijigamba Mkanwa ambaye kwa sasa ana cheo cha Meja.
Polisi Mara
inakabiliwa na mchezo na BurkinaFasso ya Morogoro utakaochezwa kwenye dimba la
Jamhuri mjini Morogoro, utakaochezwa Januari 7, mchezo ambao Mkanwa anakiri
kuwa utakuwa mwepesi kwao kwani wamejiandaa vema ndio maana wameweka kambi
jijini Dar es Salaam.
Pia Mkanwa
alitoa shukrani kwa wasaidizi wake Clement Kajeli na Omar Hamis na uongozi wa
jeshi la Polisi kwa ushirikiano wanaompa kwani unafanya majukumu yake kwenda
vema bila vipingamizi.
No comments:
Post a Comment