UONGOZI wa
Chama cha Madaktari Tanzania, (TASMA) kimekipongeza chama cha Waamuzi Taifa
(FRAT) kwa kujali afya za wanachama wao kwani ndicho chama pekee nchini ambacho
kinafuatilia kwa makini afya za wanachama.
Akizungumza
jijinI, Katibu wa TASMA, Nassor Matuzya, alisema katika vyote vya michezo
ambavyo vinatakiwa kuhudumiwa na TASMA, chama pekee ambbacho kinawapima
wanachama wake kabla ya kufanya mitihani ya utimamu ni FRAT ikifuatwa na TFF
tu.
“Naipongeza
FRAT kwani imekuwa makini kuhakikisha hakuna mwanachama wake ambaye ambaye
anaingia kwenye mitihani ya utimamu bila kuchunguzwa afya ikifuatiwa na TFF
lakini vyama vingine bado havijaleta taarifa wala kushirikiana nasi katika
jambo lolote”, alisema Matuzya.
Pia
aliwataka viongozi wa vyama vyote vya michezo kuhakikisha wanawatumia madaktari
ambao ni wanachama wa TASMA kwani wamepitia mafunzo ya tiba ya wanamichezo bada
ya kuchukuwa madaktari ambao hawana elimu kitu ambacho ni hatari kwa afya ya
mchezaji.
Vyama
ambavyo alivitaja vipo na vinaendesha mashindano lakini havishikiani na TASMA
ni CHANETA, Vyama vyote vya ngumi, Chama cha Mchezo wa kikapu, Chama cha Mchezo
wa Wavu, Kareti, Kuogelea, Magongo na mingine mingi.
Matuzya
alisema ifike mahali sasa viongozi waweke mbele kuthamini afya za wana michezo
kwa kutumia madaktari wenye sifa kwani ni moja ya majukumu ya TASMA ya
kuyatekeleza.
Pia
alivipongeza klabu za Simba, Yanga na Azam kwa kuwa mfano wa kuigwa katika
kupima afya za wachezaji wake.
No comments:
Post a Comment