Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, October 1, 2014

WENGER ATAKA ARSENAL "IKAZE" NA KUIFUNGA GALATASARAY LEO

 

Arsene Wenger ameipa changamoto Arsenal kupiga kiki Msimu wao unaosuasua kwa kuwatandika Vigogo wa Uturuki Galatasaray Jumatano Usiku Uwanjani Emirates watakapocheza Mechi ya Kundi D la UEFA CHAMPIONS LIGI.
Wenger amefadhaishwa na kikosi chake ambacho kimezorota kiasi cha kushinda mechi moja tu kati ya 6 walizocheza mwisho.
Mechi ya UCL ni ya pili kwa Arsenal katika Kundi D baada ya kufungwa Mechi ya kwanza huko Germany Bao 2-0 na Borussia Dortmund.
Galatasaray wao walianza kwa Sare ya Nyumbani ya Bao 1-1 na RSC Anderlecht. 

Kwenye Mechi yao ya mwisho hapo Jumamosi, Arsenal walishindwa kuutumia umiliki wao mkubwa wa Mpira kuzaa Magoli walipotoka Sare ya 1-1 na Mahasimu wao wakubwa Tottenham na pia Mechi hiyo iliwapa majanga pale Mastaa wao, Aaron Ramsey, Nahodha Mikel Arteta na Jack Wilshere, wote kuumia na wataikosa Mechi hii ya Jumatano ingawa upo uwezekano Wilshere akawa fiti.
Wenger amelalama: “Kitu kizuri ni kuwa bado hatujafungwa kwenye Ligi lakini kibaya ni kuwa hatukushinda katika Mechi mbili ambazo tulistahili na hivyo tumepoteza Pointi 4 bure.”

Aliongeza: “Lazima tudumishwe kutofungwa lakini pia sasa inabidi tuanze kushinda badala ya Droo. Ushindi uanze kwa Mechi hizi.”

No comments:

Post a Comment