KOCHA
MKUU wa Barcelona, Luis Enriqye, amethibitisha kuwa Straika wao mpya
Luis Surez atacheza Mechi ya kugombea Gamper Trophy dhidi ya Club Leon
ya Mexico Jumatatu Agosti 18.
Suarez alianza Mazoezi na Klabu yake mpya Barcelona kuanzia Ijumaa mara baada ya Mahakama ya Usuluhishi Michezoni, CAS [Court of Arbitration for Sport] kupunguza Adhabu yake ya Kifungo cha Miezi Minne ambacho pia kilimkataza kufanya Mazoezi na kumruhusu kufanya Mazoezi na pia kucheza Mechi za Kirafiki.
Luis Enrique amesema: “Luis Suarez atacheza kwa Dakika kadhaa Jumatatu kwenye Kombe la Gamper. Kwenye vipindi viwili vya Mazoezi ameonyesha ana kipaji kikubwa. Yeye anaonekana ndie Mchezaji tulikuwa tukimtafuta.”
Suarez aliadhibiwa na FIFA huko Brazil Mwezi Juni baada ya kumng’ata Meno Beki wa Italy, Giorgio Chiellini, wakati wa Mechi ya Kundi D la Fainali za Kombe la Dunia kati ya Uruguay na Italy.
Pamoja na Kifungo hicho cha Miezi Minne kilichamzuia kushiriki kwenye shughuli yeyote ya Soka, Suarez pia alifungiwa kutocheza Mechi 9 za Uruguay na kupigwa Faini Pauni 66,000.
Kifungo cha Miezi Minne kitamalizika Oktoba 26 na Mechi yake ya kwanza ya Mashindano inaweza kuwa hapo Oktoba 29 wakati Barcelona itacheza Mechi ya La Liga na Real Madrid.Msimu wa La Liga unaanza Agosti 24 na Barcelona inaanza na Elche.

No comments:
Post a Comment